Ads

MANISPAA YA KIGAMBONI YAPITISHA BAJETI,STANDI YA MABASI FERRY BADO HAKIJAELEWEKA

 


Mwamba wa habari

Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imesema imewaka vipaumbele katika maaeneo muhimu kaitika bajeti yake ya  2022/2023.

Akisoma hotu ya bajeti hiyo katika Baraza ya Madiwani katika kikao maalumu cha kupitisha bajeti hiyo mwishoni mwa juma ,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Ernest Mafimbo,  amesema Manispaa hiyo imepitisha bajeti ya jumla ya shilingi Bilioni 53.8 ndani ya bajeti hiyo imejumuisha na mishahara.

Amesema sehemu kubwa ya bajeti hiyo inaenda  katika  maoneo yanayo gusa jamii mojakwa moja  na katika maendeleo wametenga jumla ya shilingi bilioni 16 ambayo yanagusa Elimu  na Afya .

Aidha bajeti hiyo imetenga asilimia 10 ya bajeti hiyo kwenda katika miundombinu ya barabara  na kuongeza kuwa suala la miundo mbinu linahitaji angalau  jumla ya shilingi bilioni 35.7 hivyo  wanajitahidi kuongeza vyanzo vya mapato.

Hata hiyo Meya huyo ameiomba Serikali kuiangalia Kigamboni kwa jicho la kipekee katika miundombinu na uwekezaji kwani bado iko nyuma ukilinganisha na Wilaya nyingine nne za mkoa wa Dar es salaa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Erasto Kiwale, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwatoa fedha za kutosha kwaajili ya  ujenzi wa madarasa  ambapo Mnispaa hiyo imeweza kujenga madarasa 38,madarasa 34 katika shule za Secondari na madarasa manne katika shule za Msingi shikizi.

Katika sekta ya Afya amesema Bajeti hii itaangalia zaidi katika mazingira magumu ya watumishi ,kuboresha vituo vya Afya na Zahanati na ujenzi wa nyumba za watumishi na pia nyumba hizo  zita jengwa kwaajili ya walimu wa shule za msingi na Sekondari.

Pamoja na Hayo Mkurugezi huyo akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari hizi kuhusu standi ya Mabasi, amesema Manispaa hiyo inajenga stand kubwa katika eneo la Geza ulole  eneo lenye ukubwa  wa hekali 9.5,  tayari wamesha wagawia maeneo wafanya biashara wadogo wadogo wameshaanza kujenga .

''Kwakweli tumekuwa na changamoto katika maeno ya kujenga stand eneo la Ferry  katika Mipango miji na miundo mbinu hatuna maeneo,  maeneo yote ni ya watu na mengine ni ya taasisi mbalimbali  ila tumekuwa tukifanya mazungumzo nao ili kusudi kuona namna gani ya kusaidia wananchi  wetu maana sote inatuhusu''Amesema 

No comments