WAZAZI WAMETAKIWA KUWALEA WATOTO KATIKA MAADILI MEMA
Na Mwandishi wetu
DAR ES SALAAM
WATOTO wa Mtaa wa Mtakatifu Marko Malamba Mawili Dayosisi ya Dar es Salaam Kanisa Anglikana Tanzania wameazimisha sikukuu ya Mikaeli na Malaika Zote huku wa
Sherehe hizo zimefanyika Leo Oktoba 5,2025 katika ibada iliyoongozwa na Kasisi wa Mtaa huo Rev.Fr.Kelvin Dismas huku mambo mbalimbalai yakiongozwa na watoto ikiwemo kusoma masomo,watoto waliosoma mistari ya moyo kutoka vifungu mbalimbali kwenye Biblia ,wameimba,wamehubiri, shairi,ngonjera,maigizo pamoja na michezo mengine mingi ambayo imewafanya watoto kufurahi na kushangilia siku hii maalum kwa ajili yao.
Akihubiri katika ibada hiyo mmoja wa watoto wa shule ya Jumapili ,Alvin Kimu amewataka wazazi kuwalea watoto katika maadili mema kuanzia watoto ili wamjue Mungu na wawe na msingi bora wa Imani.
Aidha, amesema kwamba baadhi ya wazazi wanakwenda kanisani wanawaacha watoto nyumbani kwahiyo amewaomba wazazi kuwapeleka watoto wao kanisani ili wawe Wacha Mungu.
"Katika dhama hizi wazazi wamekuwa bize kutafuta maisha huku wakiwaacha watoto wao wakilelewa na wasichana wa kazi za ndani ,wazazi wengi wanakosa muda wa kukaa na watoto huku baadhi yao wakitendewa vitendo vibaya",
Pia ametoa wito kwa wazazi kuwapatia watoto sadaka wanapokwenda kanisani ili watambue umuhimu wakumtolea Mungu maana baraka zinapatika katika utoaji.
Kwa upande wake mwalimu wa watoto,Emmanuel Ndubaa amesema sikukuu ya watoto mwaka huu imekua yatofauti sana kwani wameandaa mambo mengi tofauti na miaka iliyopita.Huu ni mwaka wa Saba tangu tuanze kusherehekea siku hii ya Mikaeli na Malaika Zote katika mtaa wetu.
Amesema tumeandaa ngojera,maigizo,ushairi ambapo katika shairi watoto wamewashukuru wazazi walezi na walimu kwa kuwafundisha vizuri na kuwaombea Mungu awazidishie
"Wazazi tunawaasa,sisi ni zawadi,
Mungu ndiye alowapa,ni vema mkaitunza,
Kwa malezi ya kikristo ya kumpendeza Mungu,
Mbinguni washangilia ,Mikael na watoto",
Naye mtoto Glory Joel aliyehudhuria ibada hiyo amesema wamefurahi sana siku hii kwani imekua yatofauti sana imetukutanisha watoto na tumefanya mambo mengi na tumejifunza na tunawashauri wazazi wetu wawalete watoto kanisani wasiwaache nyumbani ili wajifunze misingi Bora ya kumjua Mungu
Post a Comment