Ads

POSTA YAPOKEA TUZO YA UDHAMINI KAHAWA FESTIVAL 2025


Shirika la Posta Tanzania limetunukiwa tuzo ya Udhamini Bora katika kilele cha Maonesho ya Kahawa Festival 2025 yaliyofanyika kwa siku tatu mkoani Kilimanjaro kama ishara ya kutambua mchango mkubwa wa Shirika hilo katika kufanikisha maonesho hayo muhimu kwa sekta ya kilimo na biashara.  


Tuzo hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe. Raymond Mangwala kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, akiwa ni  Mgeni Rasmi kwenye kilele cha maonesho hayo na kupokelewa na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Posta, Bw. Ferdinand Kabyemela.  


Posta imetambuliwa kama mdhamini mkuu aliyewezesha shughuli mbalimbali za maonesho hayo hususan usafirishaji wa kahawa na bidhaa nyingine kutoka kwa wakulima na wajasiriamali kwenda maeneo mbalimbali nchini.  


Kupitia ushiriki wake, Posta imeendelea kuonesha dhamira ya kuwa mshirika wa kweli wa maendeleo kwa kutoa huduma bora za haraka na salama zinazogusa maisha ya Watanzania moja kwa moja.  

No comments