FATHER NKWERA ,KUZIKWA LEO WATENDAKAZI WAELEZA MAMBO YALIYOJIFICHA WAKATI WA UHAI WAKE.
MWILI wa Kiongozi wa Huduma za Maombezi Duniani Marehemu Padre Felician Venant Nkwera umewasili leo Mei16,2025 Kituoni hapo ukitokea katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi Lugalo ambako ulikuwa umehifadhiwa.
Marehemu Padre Nkwera alifariki Mei 8,2025 katika Hospitali ya TMJ JijiniDar es Salaam naa ulipelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi na Leo umepokelewa na waumini ,mapadre wa kituo hicho kwa maandamano maalum yaliyotokea katika makutano ya Barabara kutoka daraja la Kijazi Ubungo hadi Kituo cha Huduma za Maombezi.
Marehemu Padre Nkwera alikua Kiongozi wa Huduma za Maombezi toka mwaka 1969 kipindi cha Serikali ya awamu ya kwanza kwa ajili ya kuombea Nchi ya Tanzania na Dunia na watu dhidi ya majanga na matatizo mbalimbali
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mwili wa marehemu Leo Mei,16,2025, Kiongozi Msaidizi wa Huduma za Maombezi Sister Eledina Michael Ntandu amesema kwamba Marehemu Padre Nkwera alishukiwa na Mama Mtakatifu Bikira Maria huko Madunda Njombe na kumwambia kwamba anze kutoa huduma ya kuombea wenye shida mbalimbali na wa dini zote Kwa Imani zao waliweza kupokea uponjaji.
Sister Eledina Michael Ntandu amesema kwamba marehemu alianzisha vituo mbalimbali vya huduma ndani ya nchi na nje ya nchi na akiwa na msaidizi wake aliyemchagua mwaka 1987.
"Mazishi ya Marehemu Padre Nkwera yatafanyika kwa kufuata kanuni zote zikiongozwa na Mapadre wa Kanisa Katoliki kwani alitii mamlaka za kikanisa isipokuwa kutoa misa",alisema Sr Ntandu.
Aidha,amesa kwamba kazi za Marehemu Padre Nkwera kazi yake ilioneka kwa kutenda miujiza kwa kuombea wagonjwa na wenye shida na yeye hakuwa mtu wa kujitangaza kwenye vyombo vya habari.
Pia,amewatoa hofu waumini wa kituo hicho kwamba huduma itaendelea kama kawaida kwani "Kazi ya Mungu haiwezi kufa itaendelea".
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Huduma za Maombezi Deogratus Karama amesema kabla ya mwaka 1991 father hajaamriwa na Askofu wake kwamba anafanya uchunguzi alikua anaombea makanisani na nchi pamoja na majimbo yote Tanzania aliyatembele na alikua akitoa huduma na Askofu.
Alisema mchango wa kazi ya Marehemu Padre Felician Nkwera ulitambulika kijamii ulimwenguni na hata Kiongozi Mkuu wa Kipindi hicho Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili alimtunuku cheti Cha mfanyakazi Bora.
Naye MC Maxmilium Kisiwa ameeleza kwamba Marehemu Padre Nkwera atazikwa Mei 17,2025 kwahiyo waumini na waombolezaji wanatakiwa kufika kituoni hapo kuanzia saa 12:30asubuhi na Misa itaanza saa 9:00 asubuhi.
Post a Comment