AMANI NITUNU KWA TAIFA LETU TUSIKUBALI MACHAFUKO
Na mwandishi wetu
Dar es Salaam
MGOMBEA mweza wa Urais kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi,Evaline Wilbard Munisi amewataka watanzania kudumisha amani iliyopo nchini kwamba Amani ya Taifa letu ni dhamana yetu sisi wenyewe,amani ikipotea hakuna pakuipata.
Akizungumza Leo Oktoba 4,2025katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni Jimbo la Kibamba zilizofanyika katika eneo la Stendi ya Magufuli Jijini Dar es Salaam amesema kuwa tulinde amani yetu tumeiasisi kutoka enzi na enzi tusishawishike Wala kudanganyika na wanaoleta uchochezi na ushawishi Kwa ajili ya machafuko na ghasia.
"Amani ya Taifa letu ni dhamana yetu sisi wenyewe,amani ikipotea hakuna pakuipata,nchi tulizopakana naizo zote wanakimbilia kwetu,Sasa sisi kikinuka kama ambavyo wanasema watakinukisha hatuna pa kwenda,tuilinde amani yetu tumeiasisi kutoka enzi na enzi msishawishike Wala msidanganyike na wanaoleta uchochezi na ushawishi kwa ajili ya machafuko na ghasia",amesema
Amani ya nchi ndio dhamana ya mwananchi mwenyewe lakini wewe mwenyewe usishawishike tumejipanga kuanzisha mijadala ya amani,mijadala ya muafaka na itaanzia ngazi ya kata,Jimbo Hadi Taifa na vijana watashiriki kikamilifu na kutakua na utaratibu na masharti mepesi kwa vijana kujiunga na jeshi la kujenga Taifa(JKT) kwani ili kuwajenga vijana kuwa wakakamavu na maadili mema sasa hivi tunaona mmomonyoko wa maadili na wakulaumiwa ni sisi wazazi kwa sababu vijana tumewaacha na kuwasahau na masharti yamekuwa mengi pamoja na vigezo vingi ambavyo vinawashinda kujiunga huko,endapo NCCR-Mageuzi kitashika dola watahakikisha vijana wote wenye sifa watajiunga bila kujali umri kikubwa ni vijana wawe na maadili kwani mafundisho wanayoyapata yanawajenga kuwa wazalendo na watii.
Aidha ,amesema kwamba wananchi wakichague chama Cha NCCR- Mageuzi kwa kumpigia kura Mgombea Urais Ambar Haji Khamis ,huku akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Kibamba ,Lightness Laizer pamoja na mgombea Udiwani wa Kata ya Mbezi,Talick Abdul Rahman Saad.
Kampeni hizi ni muendelezo wa kampeni zinazoendelea kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29,2025 huku akiwataka wananchi kukipa ushindi wa kishindo chama hicho wagombea wao kwa nafasi ya urais,ubunge na Udiwani
Mgombea Mwenza Munisi amesema kwamba tunataka kuona mageuzi katika suala Zima la Uchumi Jumuishi ambapo tutajumuisha wananchi wote wenye sifa watashiriki harakati za kiuchumi katika maeneo yote ili kuingiza Pato la Taifa pamoja na wananchi wanufaike katika ajira za muda mrefu na mfupi na watakaopata ajira za kudumu kulingana na weledi na elimu na sifa zinazohitajika mahali hapo.
"Hatutaruhusu wageni waje kunufaika na maeneo yetu ya vitega uchumi kwani wazawa wanapaswa kunufaika lakini mnawekewa masharti magumu hata Kodi mnashindwa wanakuja kunufaika wageni badala ya wazawa.
Sanjari na hayo amesema kwamba tutahakikisha watanzania wananufaika na maliasili zilizopo kwani tutaboresha na kuvumbua maliasili ili ziwanufaishe watanzania na si mafisadi.
Sambamba na hayo pia amesema kwamba wataboresha huduma ya afya ya mama na mtoto pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa dawa katika hospitali na kuboresha maslihi ya wauguzi na madaktari ili kukomesha mazingira ya kuomba rushwa huku mishahara ikitoka kwa wakati na kuongezeka Kila mwaka.
Aliendelea kwamba watahakikisha wanaboresha maslahi kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuwawekea mazingira mazuri ya kuishi kwa hadhi yake na cheo chake.
Alimalizia kwa kusema kwamba endapo NCCR- Mageuzi watapata ridhaa ya kuongoza nchi hii watahakikisha Jimbo la Kibamba kupitia Mbunge wao watajenga soko kubwa ili kuwarahisishia wakazi wa eneo Hilo na wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa urahisi pamoja kuhakikisha Barabara zinakuwa na lami.
Kwa upande wake Mgombea Ubunge Jimbo la Kibamba ,Lightness Laizer amesema kwamba atahakikisha anatekeleza Ilani ya Chama hicho pamoja na kuboresha maisha ya wananchi .
Aidha amesema kwamba kumekuwa na changamoto kubwa ya afya ya akili hii inasababishwa na ugumu wa maisha Kwa watu kubaka,ukatili na kujiua kitu ambacho akili inafikia muda haifanyi kazi vizuri hivyo mkinipa ridhaa chama hiki tutaboresha maisha na kukomesha ukatili
Naye Mgombea Udiwani Kata ya Mbezi,Talick Abdul Rahman Saad amesema kwamba endapo mtanipa ridhaa yakuwa diwani nitahakikisha changamoto za Barabara,maji na afya zinatekelezwa lakini pia nitahakikisha na kusimamia fursa za vijana na kukuza vipaji vyao
Post a Comment