Ads

LHRC NA UBALOZI WA NORWAY WASAINI MKATABA ,MAMBO KADHAA YATAJWA.

 



UBALOZI wa Norway umesaini mkataba mpya wa miaka mitatu na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ili kuendeleza Kazi  za kutetea haki na demokrasia kwa Watanzania


Mkataba huo wa makubaliano kati ya Norway na LHRC umesainiwa leo 8 Septemba  8,2025 Jijini Dar es Salaam. Katika mkataba huo Norway itasaidia LHRC kwa zaidi ya shilingi bilioni 7.


 “Makubaliano haya yanaonyesha dhamira ya muda mrefu ya Norway kutetea haki za binadamu nchini Tanzania kwa kuunga mkono  juhudi za LHRC, kwa kuchangia jamii yenye haki za kisiasa, maridhiano, uwezeshaji wa wanawake na uhuru wa kujieleza, ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.” amesema Balozi  Tone Tinnes  


Aidha  amesema kwamba  mashirika ya kiraia yana nafasi muhimu sana ya kusaidia jamii kwa hali na mali katika changamoto zinazowakabili hasa katika utetezi


“Haki za kisiasa na maridhiano ni msingi wa imani na utulivu. Demokrasia imara inategemea uhuru wa kujieleza na sauti huru, na Norway inajivunia kuunga mkono kazi za LHRC kulinda thamani hizi.”


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji  LHRC ,Fulgence Massawe amesema msaada huu umekuwa msaada mkubwa kwa jamii utasaidia katika shughuli mbalimbali hasa za kusaidia jamii kwa kuleta mageuzi ya sera na kukuza jamii jumuishi na yenye usawa,tunaishukuru Norway kwa dhamira hii kwani ushirikiank huu umetuwezeaha kusikikakwa niaba ya wanyonge ili kuleta haki na heshima kwa wote


 LHRC itaendelea kushughulikia mageuzi ya kisheria, masuala ya uchaguzi, haki za wanawake na watoto, pamoja na kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi.


No comments