Mstahiki Meya Temeke kuanza na utekelezaji wa ahadi za Rais Dkt. Samia
Na Francisco Peter, Dar es Salaam
Diwani wa Kata ya Tandika, Uzairu Abdul Athumani, amepitishwa na baraza la madiwani manispaa ya Temeke kuwa Mstahiki Meya wa halmashauri hiyo .
Mstahiki Meya Uzairu amesema katika uongozi wake atazingatia vipaumbele vinne: kwanza, utekelezaji wa ahadi za Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya siku 100 za kwanza; pili, kuhakikisha matumizi sahihi ya rasilimali watu na fedha; tatu, kufuatilia na kuhakikisha mipango na miradi inatekelezwa kwa wakati sahihi; na mwisho, kuhakikisha vijana wanapewa vipaumbele katika nyanja zote.
Wakati jambo linguine ikiwa mikakati ya kuhakikisha wanashirikishwa na wanasikilizwa ili kuchangia maendeleo ya Taifa.
Kikao hicho maalumu cha kumpitisha , kilifanyika katika ofisi za halmashauri zilizopo Wilaya ya Temeke, mkoani Dar es Salaam.
"Napenda kuongoza kwa mafanikio hivyo naahidi kuongoza almashauri ya viwango nimepanga kusimamia utendaji uliotukuka kuleta maendeleo ,"amesema Meya Uzairu.
Kipaumbele kingine ameeleza kuwa atahakikisha anasimamia dira ya utendaji wa baraza ambapo na kuhakikisha madiwani wanasimamia kutekeleza Hadi zao.
Uchaguzi huo uliongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke,Nicodemus Tambo, ambapo ulitanguliwa na uapisho wa madiwani 33 wateule wa halmashauri ya Temeke pamoja na viapo vya ahadi ya utekelezaji wa majukumu yao.
Halikadhalika, diwani wa viti maalumu, Nuru Cassian Bayingana, aliibuka kuwa Naibu Meya wa halmashauri hiyo kwa kura zote 33 za “ndiyo” zilizopigwa pia na madiwani.
Cassian amesema kuwa atashirikiana vema na makundi ya wanaweke na vijana kuhakikisha huduma na fursa zinazowahusu zinawafikia kwa wakati.
Kikao hicho pia kilipokea taarifa ya Mkurugenzi Jomaary Satura na kuwataka madiwani kufanya kazi kwa bidii.
Naye Katibu wa Mwenezi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya hiyo ya Temeke Ally Mussa alisema kuwa madiwani wote wlioapishwa waende kuchapakazi na kuwa jina mheshimiwa ambapo tayari wameanza kulitumia liwafanye chachu ya kuwatumikia wananchi ilikuepuka kulitumikia kwa kutamba bila kuwa na mafanikio ya kuchapakazi.
"Madiwani mkasimamie mapato na kusimamia watumishi na kuepuka migogoro," amesema Mussa.
Baraza hilo katika moja ya kamati zake jina la Mwanaidi Abdalla lilichaguliwa uongoza kwenye bodi ya Ajira ambayo inatarajiwa kutoa faida za kimkakati.
Pia kamati ya fedha yenyewe kimsingi uongozwa na Meya na wajumbe wake ni Naibu Meya pamoja na wabunge ambapo katika halmashauri hiyo inawabunge wa majimbo ya Mbagala, Chamanzi na Temeke.

Post a Comment