MSAJILI WA HAZINA AWAKUMBUSHA WATUMISHI WA MASHIRIKA KUHUSU KUPIGA KURA
Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) inapenda kuwakumbusha na kuwasisitiza watumishi wote wa umma waliopo katika taasisi na mashirika ya umma kote nchini kutumia haki yao ya msingi ya kikatiba kwa kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Oktoba 27,2025 Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Usimamizi Mashirika ya Kibiashara ,Lightness Mauki amesema kushiriki kwa wingi katika uchaguzi huu,watumishi wa umma wataendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kuimarisha utawala Bora,uchumi emdelevu,na ustawi wa wananchi
Aidha,amesema Ofisi inatoa wito kwa wakuu wa taasisi na mashirika ya umma kuhakikisha kwamba watumishi wao wanapatiwa fursa ya kutekeleza haki hii muhimu bila kuathiri majukumu yao ya kikazi, kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.
Ofisi ya Msajili wa Hazina, imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Msajili wa Hazina (Madaraka na Majukumu), Sura ya 370, ina jukumu la kusimamia na kuendeleza uwekezaji wa Serikali katika taasisi na mashirika ya umma na kampuni ambazo Serikali ina hisa au maslahi. Pamoja na majukumu hayo, Ofisi pia inahakikisha usimamizi bora na ustawi wa rasilimaliwatu waliopo katika taasisi hizo ili kuimarisha uwajibikaji, uadilifu, na mchango wao kwa maendeleo ya Taifa.
Katika kuzingatia majukumu hayo, Ofisi inawakumbusha watumishi wote katika taasisi na mashirika ya umma kwamba:
1. Kushiriki uchaguzi ni wajibu wa kiraia unaojenga demokrasia, umoja, na uthabiti wa Taifa.
2. Kupiga kura ni chombo cha mabadiliko chanya, kinachowawezesha wananchi kuchagua viongozi wenye maono, uadilifu, na uwajibikaji.
3. Ushiriki mkubwa wa watumishi wa umma unaonesha mfano wa uzalendo, nidhamu ya kitaifa, na uelewa wa majukumu ya kikatiba

Post a Comment