HUU NDIYO MCHANGO MKUBWA WA SERIKALI SEKTA YA AFYA NCHINI
Na Mwandishi wetu
DAR ES SALAAM
MABALOZI zaidi ya 11 kutoka nchi mbalimbali pamoja na washiriki zaidi ya 300 Toka nchi mbalimbali duniani wameshiriki mkutano wa 12 waAfya Tanzania( 12th Tanzania Health Summit) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa Leo Oktoba 1,2025 Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi na Mwanzilishi wa Tanzania Health Summit,Dr.Chakou H.Tindwa wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kwamba summit ina miaka 12 na tumebahatika kupitia awamu tatu za uongozi Toka Rais Kikwete, Hayati John Pombe Magufuli na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan
Aidha amesema tunapotimiza miaka 12 tunayo maeneo yakujipima katika utendaji wetu ambapo eneo la kwanza ni washiriki katika summit zilizopita hasa idadi ya washiriki ilikua mia 500 Kwa Kila mwaka wakati Rais Samia anaingia madarakani lakini tangu aingie madarakani idadi ya washiriki imeongezeka Hadi 1500 kwa mkutano wa mwaka Jana uliofanyika Zanzibar na mwaka huu 2025 zaidi ya washiriki 1700 Kuna mafanikio zaidi ya mara tatu .
"Wanaposhiriki watu ujue Kuna mchango mkubwa sana wa serikali kitendo hiki kimetufanya sisi kama summit tuone mchango mkubwa wa serikali lakini pia katika makusanyo yameongezeka mara Dufu na hata uchumi wa summit umeongezeka na hata katika kujitegemea umekua vizuri",amesema Dr.Tindwa
"Miaka ya zamani Mimi kama mwanzilishi nilikua nachangia fedha kutoka mfukoni lakini tangu aingie madarakani Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kweli sijatoa hata Senti Tano ya kusaidia summit ,Sasa inajiendesha yenyewe",amesema
Hata hivyo inatokana na Mama Samia kufungua mipaka ya nchi kwani tangu aingie madarakani idadi ya washiriki imeongezeka hapo nyuma washiriki toka nje ya nchi ni kama 15 Hadi 20 lakini tangu aingie madarakani ni zaidi ya 150 Hadi 200 na mabalozi miaka ya huko nyuma ilikua 1 au wawili.
Sanjari na hayo Kwa mara ya kwanza serikali imechangia summit kwa kufahamu umuhimu wa mkutano huu na mijadala na mawazo ya watu katika kuboresha sekta ya Afya,Kwa mara ya kwanza tumepokea mchango kutoka wizara ya afya, hivyo tunaona mchango wa serikali unavyoendelea kuimarika,tunaona msaada mkubwa kutoka kwa Rais Dkt.Mwinyi na Rais Dkt.Samia hivyo tunawatakia Kila la heri katika Uchaguzi Mkuu"sisi kama summit tungekuwa tunachagua basi kula zote tungempa Dkt.Samia",
Pia kama mnavyofahamu mwaka huu serikali ya Marekani imepunguza sana misaada kwa hali ya kawaida bila kuwa na uongozi imara nchi yetu ingeyumba lakini hutujasikia kwamba Kuna upungufu wa dawa,Wala hospitali kufungwa hakuna jambo lolote lililotokea kwa sababu hiyo kutokana na uwezo wa kiongozi aliokuwa nao.
"Sisi Kama Summit tunatambua na kuthamini mchango wa Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan hivyo tutaendelea kushirikiana nae",amesema Mwenyekiti Dr.Tindwa
Post a Comment