TANZANIA NA HUNGARY ZASAINI MKATABA KUSAMBAZA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA MKOA WA KAGERA
Serikali ya Tanzania na Hungary, Wamesaini hati ya Mkataba wa Mashirikiano kuhusu Mashirikiano ya Mradi wa Usambazaji Maji kutoka Ziwa Victoria katika Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.
Hati hiyo ya Makubaliano ni kati Kampuni ya MeOut ya Hungary na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo ya Tanzania Kuhusu masuala ya teknolojia ya kilimo.
Akizungumza Leo Septemba 29 Jijini Dar es salaam mara baada ya hafla ya hiyo ya Utiaji Saini Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabiti Kombo.
Amesema Hungary ni Nchi iliyoendelea Sana katika teknolojia ya Maji hivyo Biharamulo inakwenda kutatuliwa changamoto ya upatikanaji wa Maji.
Hata hivyo amesema Nchi hiyo imekuwa na Mashirikiano ya muda mrefu kwani wamekuwa wakitoa Ufadhili kwa Wanafunzi 30 Kila Mwaka katika fani mbalimbali na ili kudumisha mahusiano hayo wamefungua Ubalozi wao hapa Nchini Tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary, Mhe. Péter Szijjártó amewasili nchini Tanzania Septemba 29, 2025 kwa ziara ya kikazi ya siku moja itakayoambatana na matukio mbalimbali ikiwemo Kusini Mkataba na kufungua Ubalozi wao Tanzania , itakuwa tija kubwa Kujenga Diplomasia baina ya Nchi hizi mbili
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mhe. Szijjártó’ amepokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi na viongozi wengine waandamizi kutoka Serikalini.
Kwa Upande wake TCCA Vincent Minja Amesema kwamba Nchi ya Hungary imeendelea Sana katika masuala ya teknolojia ya kilimo hivyo kwa kuwa Tanzania Kilimo ni uti wa mgongo Mashirikiano hayo yataleta tijakwa Wakulima ili Kulima Kilimo Biashara cha kisasa ili kujikwamua na umaskini
Post a Comment