Ads

HILI HAPA TAMKO LA GCAP KUHUSU MIAKA 10 YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs).





Na Angelina Mganga

MTANDAO wa kampeni ya kupambana na umaskini duniani Tawi  la Tanzania(GCAP) katika kuadhimisha miaka kumi ya utekelezaji wa malengo Endelevu ya Dunia(SDGs) kupitia Mratibu wa Taifa 2a Shirika la SAHRiNGON Tanzania Chapter na GCAP Tanzania Coalition,Martina Kabisana amesema huu ni mtandao mkubwa wa kiamataifa unaounganisha zaidi ya mashirika 11000 ya kiraia katika  zaidi ya nchi 70 .


GCAP imejikita zaidi katika umuhimu wa kupanua elimu ya msingi,kuboresha huduma za afya na kuimarisha miundombinukama hatua muhimu za kupambana na umaskini duniani.


Akizungumza na waandishi wa habari Leo septemba 25,2025 Jijini Dar es Salaam,tunapotimiza miaka 10 ya SDGs,Tanzania pia imekamilisha Dira ya Maendeleo ya 2025 Hadi 2050inalenga kujenga uchumi shindani, jumuishi na endelevu. Aliongeza kuwa dira hiyo inalenga kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wastani wa zaidi ya asilimia 8, kuongeza umri wa kuishi hadi miaka 75, na kuhakikisha kaya zaidi ya asilimia 90 zinapata huduma ya nishati.


Aidha,amesema kwamba pamoja na mafanikio yaliyopatikana na mipango madhubuti ya maendeleo, bado tunakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo kiwango kikubwa cha umasikini, ukosefu wa ajira kwa vijana, kutokuwepo kwa usawa wa kijamii, mabadiliko ya tabianchi, pamoja na masuala ya uongozi na uwajibikaji


Naye Rosemary Mwaipopo kutoka Global Call to Action Against Poverty (GCAP) ametoa wito kwa serikali ya Tanzania kuhakikisha inalinda haki za raia, kuimarisha misingi ya haki za binadamu, kusimamia utawala bora, na kuongeza uwekezaji katika ulinzi wa jamii. 


Aliongeza kuwa sera na bajeti za kitaifa zinapaswa kuelekezwa katika kujenga uchumi jumuishi na kutoa ajira zenye staha kwa vijana.


 Hata hivyo katika hatua nyingine aliwahimiza wadau wa maendeleo, sekta binafsi, Umoja wa Mataifa, taasisi za kikanda na asasi za kiraia kuendelea kupaza sauti za wananchi—hasa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili kuharakisha utekelezaji wa SDGs nchini Tanzania.

No comments