TASAC:Sekta ya bahari ndiyo unayoongoza kwa mchango mkubwa kiuchumi
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC) Mohamed Salum amesema kwamba Sekta ya Usafiri Majini ina uhaba mkubwa wa mabahari,hivyo amewaomba Wananchi kuchangamkia fursa hiy kwa kuwapeleka watoto wao kusomea sekta hiyo.
Taarifa hiyo ameitoa leo Julai 7,2025 wakati alipotembelea Banda la Wakala huo kwenye maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es salaam.
Aidha amesema kwamba Vijana wengi wamekua wakisomea sekta zingine na kuacha Sekta ya Bahari ambayo amedai ina fursa nyingi za ajira,nakuwashauri wazazi na Walezi kuwahamasisha watoto wao kusomea sekta ya Bahari ikiwemo ubaharia.
"TASAC imeshiriki maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara kwa lengo kutoa Elimu juu ya majukumu ya Wakala huu ikiwemo kudhibiti usafiri majini pamoja na kuchagiza sekta ya usafiri Majini."amesema
Nakuongeza kuwa "Ukitembelea Banda letu utajua fursa zinazopakana ikiwemo mfuko wa mafunzo ya Sekta ya Bahari,pia kwa upande wa wanawake wanapata fursa ya kusomea sekta ya Bahari "amesema Mkurugenzi Mkuu huyo wa TASAC
Amesema kuwa Wakala huo umekua ukisajili vyombo vya majini nakuvipa cheti cha ubora ,kwa ajili ya kufanya shughuli zake majini,ikiwa lengo ni kudhibiti sekta ya usafiri Majini.
Ameongeza kuwa kupitia Wataalamu wake imekua ikifanya ukaguzi wa Meli za kimataifa zinazoingia nchini,pamoja na uwanda mzima wa Bahari ikiwemo kutoa taarifa ya uokoaji,hali ya hewa,na taarifa kwa wavuvi ili kuweza kuchukua tahadhari,nakuhakikisha Bahari inabaki safi.
Mkurugenzi Mkuu huyo wa TASAC ameendelea kusema kwamba Wakala huo umekua ukisimamia usalama wa bandari,kutoa leseni za bandari, kusimamia shughuli zote za ujenzi wa bandari.
"Wanaotoa huduma bandarini mfano DP World,au TPA tunawawekea viwango vya utendaji wao wa kazi nakuangalia utendaji wao kama unaathiri shughuli za upakiaji na upakuaji wa mizigo,pamoja na usalama kwenye maeneo yote ya bandari.
Post a Comment