Ads

IGP WAMBURA ATEMBELEA BANDA LA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI SABASABA

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camilius Wambura tarehe 6 Julai, 2025 ametembelea Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.


Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inashiriki maonesho hayo kwa  kutoa  huduma ya Elimu ya Sheria, Ushauri wa Kisheria, Kughulikia Malalamiko na Utatuzi wa Migogoro, ambapo Banda la Ofisi liko katika Mtaa wa Media, Hema la Jakaya Kikwete banda namba 24.


Maonesho ya Sabasaba yenye kauli mbinu ya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Fahari ya Tanzania yalianza tarehe 28 Juni , 2025 na yanatarajiwa kumalizika tarehe 13 Julai, 2025.IGP




No comments