Ads

TCCIA YAJA MAPINDUZi MAKUBWA YAKIDIJITALI

 


Na mwandishi wetu


DAR ES SALAAM 

MENEJA wa Viwanda wa  Tanzania Chamber of Commerce Industrial and Agriculture(TCCIA) ,Ezekiel Karatano anawakaribisha watanzania kutembele katika Banda lao kwenye maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (SABASABA) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius K.Nyerere Jijini Dar es Salaam.


Ameyabainisha hayo Leo Julai 5,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kwamba amewakaribisha kuja kujionea bidhaa mbalimbali zinazopatikana katika Banda lao na huduma wanazozitoa.


Aidha ,amesema kwamba TCCIA wamejipanga katika mapinduzi ya kidijitali kwani yanakwenda sambamba na kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu.


Ameongelea huduma maalum (certificate of original) huduma  ambayo inamwezesha  mfanyabiashara ama mzalishaji wa ndani ya nchi ambaye anapeleka bidhaa zake nje ,huduma ambayo Ina mpa uwezo wa kupata punguzo la tozo kwa asilimia kubwa kutokana na , Kanda za kibiashara ambazo Serikali imeungana nazo.


Ameongeza kwamba Kuna Kanda tatu ambazo ni Afrika Mashariki,Kanda ya Afrika na SADC ambapo mfanyabiashara ama mzalishaji ambaye anafanya biashara ambaye yupo ndani ya nchi anapeleka biashara zake nje ya nchi anapata punguzo kubwa la tozo ili apate punguzo anatakiwa kupata cheti cha asilia , kwahiyo TCCIA imekuja na mapinduzi ya kidijitali yakutoa cheti cha asilia.

Mwanzo ilikua inachukua siku tatu hadi nne mfanyabiashara kupata cheti ambacho kilikua katika mfumo wa karatasi lakini sasa hivi mteja alipo ndani ya dakika kumi anapata cheti chake kidijitari na hii inarahisisha mfanyabiashara kusafirisha bidhaa zake na hapo mwanzo kusafirisha cheti ni lazima aende na cheti chake lakini kwa kuwa mifumo inasomana kwa hiyo mteja hana sababu yakutembea na cheti kwa kuwa kipo kwenye dijiti kwahiyo kinasambaa kwahiyo Kila mpaka atakaofika akiweka namba tu cheti chake  atakipata  pale hivyo inapunguza muda kwa wafanyabiashara kwa kupata vyeti kwa kuongeza ufanisi wa biashara zao lakini pia serikali kujipatia kipato





No comments