Ads

MBUNGE BONNAH ASIKIA KILIO CHA DARAJA WANANCHI WA BONYOKWA .



Na Heri Shaaban (Segerea)

MBUNGE wa jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli, amesikia kilio cha wananchi wa Kata ya Bonyokwa wilayani Ilala walioondokewa na daraja la  muda kufuatia kuondoka na mafuriko ya  mvua za masika na kukata mawasiliano ya Barabara Kinyerezi  kuelekea  bonyokwa  Kimara. 


Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya kutembelea miundombinu iliyokumbwa na mafuriko Mbenge wa jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli alisema aliona video ikisambaa kuekezea eneo hilo ambalo lipo katika ujenzi wa daraja la kisasa likionyesha daraja la muda lineondoka hivyo kulazimika kufanya ziara ya ghafla. 


"Kwanza poleni wananchi wangu kufuatia mawasiliano ya barabara yenu kukatika kufuatia kivuko kwenda na maji ya mvua za masika pia nampongeza yule aliyesambaza video mpaka ikanifikia na leo nimekuja kuonana na Mkandarasi aliyekabidhiwa mradi huo pamoja na Meneja wa TANROADS ambao ndio wasimamizi wakuu wa barabara bonyokwa Kimara  "alisema  Bonah. 


Mbunge Bonnah, alisema changamoto kubwa jimbo la Segerea mvua inanyesha  Kisarawe mkoa wa Pwani na Kibaha maji yake yote yanaelekea Jimbo la Segerea ususani bonde la Mto Msimbazi linapokea maji mengi 


Alitumia nafasi hiyo kumwagiza Mkandarasi wa daraja hilo Kampuni ya Nyaza kujenga daraja la muda haraka liwe imara kwa ajili ya kuunganisha mawasiliano ya eneo hilo Kinyerezi, Bonyokwa kuelekea Kimara wilayani Ubungo. 


Aidha Mbunge Bonnah alisema barabara hiyo pamoja na daraja ni muhimu sana  kwa wananchi inatumika na wilayani Ilala, Wilaya ya ubungo na inaunganisha mawasiliano makubwa ikikamilika itatatua changamoto kwa wananchi wa eneo hilo na uchumi utapanda  na maeneo yao yatakuwa na thamani mara barabara hiyo itakapokamilika .


Mhandisi wa TANROADS Rajabu Kiamba alisema TANROADS imekabidhi kazi ya ujenzi wa barabara ya Kimara Bonyokwa na daraja lake ambapo pia jukumu la kutengeza barabara ya muda lipo katika mkataba wa Mkandarasi wa Kampuni hiyo ya Nyanza .


Mkandarasi wa ujenzi wa barabara hiyo Kampuni ya Nyanza Gribert Bahasha alisema barabara kwa sasa Kimara Bonyokwa imefungwa kwa ajili ya usalama wa wananchi pamoja na wanaotumia vyombo vya moto kutokana na mvua za masika kubwa bonde hilo linabeba maji mengi wasije wakaenda na maji.


Mkandarasi Grubert alisema kwa saaa wapo katika taratibu za kujenga daraja kubwa la kisasa wanasubili mvua ziweze kupungua ujenzi wake uweze kuanza wa daraja kubwa.


"Mradi wa ujenzi wa barabara hiyo ya Kimara bonyokwa walikabidhiwa mwaka 2024 mara baada kukabidhiwa wakaondoa dsraja la chuma ili daraja jipya ujezi wake uwanze rasmi  wakati ujenzi unaendelea mafutiko ya mvua za Masika zimeondoa daraja ls muda "alisema Gribert.


Katika ziara hiyo mbunge wa Segerea  kuangalia miundombinu ya jimbo alitenbelea daraja kata ya Bonyokwa ,Kinyerezi eneo Kanga ,kata ya Liwiti na Kipawa .

No comments