Shirika la kupambana na unyanyasaji Kijinsia ''Mulika Community '' lazinduliwa
Na Heri Shaaban (CHANIKA)
SHIRIKA lisilo la kiserikali la kusaidia jamii na waathirika wa unyanyaaaji kijinsia limezinduliwa rasmi na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jery Silaa.
Akisoma taarifa ya shirika la Mulika Community Mwenyekiti wa shirika hilo Saida Mavumbi Ally alisema malengo ya shirika hilo kuwaunganisha waanga wa kijinsia zote na kuwapa mafunzo ya afya ya akili ,ikiwemo kutoa misaada wa kisheria kwa ajili ya kulinda haki na utu wa Jamii husika .
" Leo ni siku ya uzinduzi wa shirika letu la mulika linaloshughulikia maswala ya kikatili kijinsia ambalo litakuwa linaisaidia Serikali kukomesha vitendo vya kijinsia na ukatili kwa jamii pamoja na kuhamasisha na kutoa tahadhari juu ya mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na kuweka sawa mazingira ikiwemo kupanda miti katika taasisi za Serikali na shuleni "alisema Saida
Mwenyekiti Saida alisema pia majukumu yao mengine shirika hilo kutoa elimu mtambuka yenye kuleta tija katika jamii iliyoathirika ili kutambua haki zao hususani haki za watoto wadogo ,haki za wafanyakazi majumbani ,ikiwemo kupata elimu na haki ya kupewa uhuru wa kwenda kuchagua viongozi.
Pia alisema shirika la Mulika dhumuni lao lingine kwa kusaidia jamii kuwajengea uwezo imara makundi ambayo yamepitia changamoto ya kutengwa na jamii na kuteswa vibaya ikiwemo vipigo na kunyimwa haki za msingi.
Akizungumzia mikakati ya shirika hilo katika kusaidia jamii ikiwemo kutoa mafunzo ya ukatili wa kijinsia na kutunza mazingira, pamoja na kutoa mafunzo ya ujuzi wa ushonaji nguo utengezaji wa batiki ,ususi na urembo.
"Shirika letu pia linahamasisha matumizi ya Nishati safi ya kupikia kwa jamii na kutoa mafunzo ya cherahani kwa wasichana na watu wenye ulemavu wa ngozi ,wajane kwa muda wa miezi mitatu kwa wanufaika 600"alisema
Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jery Silaa,alipongeza Shirika hilo ambalo lipo jimbo la Ukonga litasaidiana na Serikali katika kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa jamii ambapo alisema atawasaidia kutafuta wadau shirika liweze kufikia malengo yake.
Mbunge Jery Silaa alikabidhi kompyuta kwa ajili ya shughuli za taasisi hiyo na kuwataka wachape kazi katika kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto na jamii kwa ujumla
Post a Comment