Ads

DIWANI ZINGIZIWA AWAKUMBUSHA WAJUMBE MACHUNGU ALIYOPITIA AKIWATETEA WANANCHI.

 



 

DIWANI wa Kata ya Zingiziwa Wilayani Ilala Maige Maganga ameeleza Wajumbe wake na Wananchi wa Zingiziwa kuwa amepigwa na Askari wa Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya mgogoro wa ardhi  wa  mpaka kutetea wananchi wake.


Diwani Maige Maganga alisema hayo leo mbele ya wananchi wake katika Mkutano Maalum ulioshirikisha Wajumbe wa mashina ,jumuiya na Viongozi wa chama cha Mapinduzi.

Maige alisena sakata la mpaka la kutetea wananchi wake mpaka wa Ardhi Kisarawe na Zingiziwa ulichukua sura mpya kufuatia ASKARI wa Kisarawe kumvamia na kumpiga bila taarifa.

"Mzigo mkubwa mpe Mnyamezi natekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM vizuri kwa kushirikiana na Mbunge wangu wa jimbo la Ukonga Jery Silaa Zingiziwa inakuwa ya Kisasa Serikali imejenga Mahakama ,Dkt Samia Suluhu Hassan amejenga Kituo cha afya cha kisasa na sekta ya elimu yote hayo ni matunda ya Serikali katika uongozi wangu "alisema Maige.

Diwani Maige alisema wananchi wa Zingiziwa hawakufanya makosa kumchagua yeye kuwa Diwani wao wamemchagua amewaletea maendeleo na .mafanikio makubwa kwa kushirikiana na Mbunge na Rais Dkt.Samia.

Alisema katika mafanikio apakosi changamoto kivuko cha Rubakaya na kwa Mama Yusuph bado anaendelea kufatilia pia katika vikao vya Baraza ili kiweze zipatikane fedha za kutengenezwa.

Pia alisema katika hatua nyingine amesema kila wakati anakuwa mkali katika kuwatetea wananchi wake wakisumbuliwa na watu wa vibari vya ujenzi amekuwa mstari wa mbele kuwasimamia wananchi wasisumbuliwe na watendaji hao ambao wanatoaga anri wananchi wasijenge mpaka wapitie taratibu .

Mwenyekiti wa ccm kata ya Zingiziwa wilayani Ilala Abdlah Mpate alizungumzia mwaka wa uchaguzi aliwataka viongozi wa chama na Jumuiya zake wafanye kazi kwa kufuata taratibu na kanuni viongozi watakaokwenda kinyume na maelekezo ya chama watachukuliwa hatua

No comments