Ads

MCHOME AMKALIA KOONI LISSU AMTAKA AKUBALI KUKOSOLEWA

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro Lembus Mchome ambaye pia ni miongoni mwa  wafuasi wa G55 amemtaka  Mwenyekiti wa  Taifa wa chama hicho Tundu Lissu kukubali kukosolewa  na wanachama ili kusimamia na kuiheshimu demokrasia anayoihubiri muda wote.

Mchome ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam mapema leo Aprili 8,2025 wakati akizugumza na waandishi wa habari ambapo amesema siasa safi ni lazima mtu akubali kukosolewa na kupokea mawazo mbadala.

Amesema baadhi ya Viongozi wa chama wamekuwa  hawakubali kukosolewa, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa Tundu Lissu licha ya kuwa muumini wa demokrasia hiyo

 "Katika  mikutano amekuwa  anasema kuna wajinga wajinga wanahoji... mwenyekiti wa chama unawaita wanachama wajinga jinga,hutaki kukosolewa umekuwa Mungu hutaki kusikiliza hoja mbadala kwa nini badala usikilize tukubali kukosolewa,naomba mwenyekiti wangu ukubali  kukosolewa ili tuweze  kujenge Chadema imara yenye nguvu,”alisisitiza Mchome.

Aidha Mchome amemuomba Msajili wa Vyama Vya Siasa  kubatilisha  maamuzi ya Baraza Kuu la Chadema lililofanyika  Januari 22 mwaka huu.

Amesema katika   kikao cha Baraza Kuu ambalo pia kilimthibitisha Katibu Mkuu  John Mnyika  pamoja na viongozi wengine wakuu saba si halali kwakuwa akidi ya wajumbe wa kikako hicho haikuwa imetimia kama inavyoelekezwa katika katiba ya chama.

 "Kiutaratibu ili kikao kianze ni lazima mwenyekiti awe na orodha lakini katika kikao kile katibu mkuu anakiri  ni kweli hawana akidi kwakuwa hawakuwa na orodha  na kama alikuwa nayo basi aipeleke kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ili aihakiki"amesema 

Pia  amemuomba msajili kubatilisha maamuzi yote yaliyofanywa Januari 22 kwakuwa hayakuwa na uhalali kulingana na aina ya wajumbe waliyoyapitisha.

No comments