TIC YA MKABIDHI HATI YA KUJENGA KIWANDA MWEKEZAJI ALIYEPATA ENEO KWA PROPERTY INTERNATIONAL.
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Kituo Cha uwekezaji nchini TIC kimesema kimeweka mazingira Bora ya uwekezaji nchini jambo ambalo limesaidia kuvutia wawekezaji kuwekeza kwaa wingi.
Hayo yamebainishwa na Afisa uwekezaji na msimamizi wa dawati la Mashariki ya kati Bwana Juma Nzima akizungumza wakati alipokuwa anakabidhi hatimiliki kwa Mwekezaji wa kampuni ya Vax Industries Ltd (Packaging Industries katika Banda la TIC katika maonesho ya biashara ya 48 ya yanayoendelea Jijini Dar es salaam.
Aidha ameitaka sekta binafsi kuendelea kushirikiana na Serikali kupitia kitu hicho kuweka akiba ya Benk ya ardhi katika maeneo yaliyo rasimishwa kwaajili ya uwekezaji .
"Leo tumefanikisha kutoa hati isiyo asili kwa Mwekezaji anayewekeza maeneo ya Kigamboni Kisarawe Il , kiwanda Cha kuchakata vifungashio na eneo hili limetoka sekta binafsi katika kampuni ya Property International tunawashukuru Sana kwaushirikiano wao kwa kuleta maeneo yao na tukayatangaza kwa wawekezaji" Alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya uuzaji viwanja ya Property International ambao ndiyo wametoa eneo la kiwanda kwa Mwekezaji huyo Bwana Abdlharim Zahran , ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuweka mazingira Bora na wezeshi kwa wawekezaji.
"Wawekezaji hawa hawaji kwa bahatimbaya mazingira yalipo ndiyo yanayowavutia kuja kuwekeza ndani ya nchi yetu na TIC wamejipanga vizuri hata Leo sikutajia kama hati hii itaweza kukabidhidhiwa ndani ya maonesho katika viwanja vya Sabasaba "Alisema.
Vilevile ametoa wito kwa sekta binafsi wenye miradi Yao kupeleka na kuisajili TIC kunamsaada mkubwa Sana kwa sababu wewekejaji wengi wamehamasishwa kuwekeza Tanzania na wanafika TIC kupata taarifa za uwekejaji .
"Unapo sajili miradi yako TIC Wana kutafutia mteja kazi inaenda kwa haraka Sana na Imani na Serikali imekuwa kubwa Sana"Alisema Mkurugenzi huyo.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Vax Industries Ltd iliyo pewa hati miliki ya eneo kiwanda kutoka Property International Bwana Viswa Vardhan Reddy , amekishuku kituo Cha uwekezaji TIC kwa kufanikisha kuwaunganisha na Property International na kupata eneo la kujenga kiwanda ambapo ameahidi kuwa karibu wataanza ujenzi .
Post a Comment