Ads

TTCL WAONGEZA UFANISI UTOAJI WA HUDUMA YA MAWASILIANO

 Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

MKURUNGEZI Mtendaji wa TTCL Pesa Lulu Mkudde amewahakikishia wananchi kuwa Shirika  la Mawasiliano Nchini( TTCL) litahakikisha  huduma za mawasiliano zinakuwa nzuri ili kuwapa fursa ya kupata huduma mbalimbali pamoja na  kujiingizia kipato kupitia mtandao huo.



Mkudde ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kuhusu shughuli zinazofanywa na shirika hilo.

Amesema ,hadi sasa Shirika  hilo limesambaza mkongo wa Taifa katika mikoa yote nchini huku zaidi ya wilaya 98 nazo zikiwa zimefikiwa na mkongo huo ambao unarahisisha mawasiliano na kuleta matokeo chanya kwenye shughuli za uchumi.

"Juhudi hizi zote zinalenga katika huduma za elimu ,afya na maendeleo kwa ujumla yanatekelezeka kidigitali katika maeneo yote nchini.

Kwa mujibu wa Mkudde Mkongo wa Taifa ni moja ya miradi ya kimkakati inayofanywa na TTCL huku akiitaja miradi mingine kuwa ni kutoa mafunzo mbalimbali, kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu.

Kuhusu ushiriki maonesho hayo amesema,katika kuunga mkono mbiu ya maonesho ya mwaka huu isemayo Tanzania ni mahalo sahihi kwa kauli Mkkude amesema, wanatumia fursa hiyo kufungua kufungua kwa kutafuta kufanya kazi zao kidigitali kwenye kuleta matokeo chanya.

Amesema katika maonesho hayo TTCL limekuja na huduma ya mtandao (WiFI T-Cafe ) ambayo imelenga kuwaondolea adhana, waziri wa habari na wataalam wa masuala ya ushauri na yeyote anayetaka kufanya kazi nje ya ofisi yake ,na kupata huduma hiyo bure.

Kwa upande wa huduma ya 'fiber nyumbani kwako amesema ' inapatikana kwa gharama nafuu na kueleza  kuwa imetolewa katika kipindi chote cha Maonesho.

"Tayari tumepokea maombi mapya mengi ,wanaohitaji huduma ambayo imekuja kuleta mapinduzi ya kuisha haraka kwa vifufushi vya kawaida, ambapo sasa shirika limeleta huduma hii ambayo inamwezesha mteja kutumia internent ambayo haina ukomo.

Aidha amesema shirika limekuja na  huduma yake ya T-Pesa ambayo inamwezesha mteja kufungua akaunti ya TTCL Pesa bila kuwa na hitaji la simu kadi.

No comments