MAMA ONGEA NA MWANAO WATOA MSAADA WA VITI MWENDO 250 KWA WAHITAJI
TAASISI ya Mama Ongea na Mwanao kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wametoa msaada wa viti mwendo 250 kwa watoto wenye mahitaji maalumu (Walemavu) ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao za kupata elimu .
"Kuna wanaume ni wazembe katika kulea Watoto wenye Ulemavu hufikia kuwa kana kuwa mtoto mwenye Ulemavu si wake, lakini mtoto akiwa na hana ulemavu anamdai mwanamke kuwa mtoto ni wake," amesema Nyerere"
Nyerere meongeza kuwa hali ya mtoto mwenye uhitaji haimzuii mtoto huyo kupata Elimu.
Amebainisha kuwa Kupata Mtoto Uhitaji ni Mipango ya Mungu nasio Mikosi na kuitaka jamii kuondoka na Dhana hiyo.
"Sisi tunahitaji kupeleka Mahitaji kwa Wenye uhitaji popote walipo hivyo tunaomba taasisi nyingine zituunge mkono," amesisitiza Steve Nyerere"
Kwa upande wake Katibu wa Taasisi Ongea na mwanao Evon Sherry amesema taasisi hiyo imetembelea mikoa mitano na kubakisha mikoa miwili kwa jili ya Viti mwendo kwa wahitaji.
Amesema kampeni ya "Baskeli ya Shule ya Mama" inalenga kumsaidia mtoto mwenye uhitaji kupata Elimu.
"Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anawasaidia wakina mama katika sekta ya Afya,Maji lakini Sisi tumeamua kumtua mama mtoto mgongoni" amesema Evon.
Post a Comment