Ads

ASKOFU KANISA LA METHODOX TANZANIA APINGA NDOA YA JINSIA MOJA

Askofu na Katibu Mkuu wa Kanisa la Methodox Tanzania Allen Siso amesema katika vitabu vya dini zote havikubaliani na ndoa za jinsia moja akitolea mfano kitabu cha Warumi 1:26 kinachosema 'hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu,hata wanawake wakabadili matumizi ya asili Kwa matumizi yasiyo ya asili,na wanaume nao vivyo hivyo'.

Katika mtazamo huo moja kwa moja ameungana na viongozi wengine wa dini nchini  kuitaka Serikali kuufungia mtandao wa Kijamii wa X ambao hapo awali ulikuwa unajulikana kama Twitter kutoka na kuruhusu maudhui ya video za ngono hususani za mapenzi jinsia moja yani Ushoga.

 Kauli hiyo imetokewa leo Juni 11, 2024 jijini Dar es salaam wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari ambapo wamesema Mungu anachukizwa na vitendo viovu ikiwemo ushoga hivyo wamesisitiza Serikali kupitia mamlaka zake mbalimbali kuona haja ya kuudhibiti mapema mtandao huo ili kutoaribu maadili kwa vijana na watoto wa Kitanzania ambao ndio Taifa la kesho.

"Mungu yupo na tunapaswa kutende yanayompendeza, Mungu ameweka njia za asili za kushiriki mapenzi na si kinyume na maumbile kufanya hivyo ni kumchukiza Mungu".

Kwa upande wake Alhaji Dkt. Abdul Selemani amesema wao kama viongozi wadini wanatumia Nafasi zao kutoa wito huo kwa Serikali, Bunge na mamlaka zote kukomesha taasisi zote zinazojihusisha kutoa mafunzo yasiofaa kwenye jamii ikiwemo mafundisho ya ushoga kuzifungia na kuwachukulia hatua kali wale wote wanaohusika ili kuwa fundisho kwa wengi.

"Tunafanya haya yote kwa manufaa ya Taifa letu,kwani Mungu akitaka kuangamiza Taifa hatachagua huyu alifanya au huyu hakufanya, kwahiyonili tusiendelee kumchukiza viongozi wadini tumeona tutumie fursa kuonya mwelekeo wa utandawazi nchini kwetu".

Naye Sheikh Hilal Kipozeo ameendela kusisitiza kuwa mtandao wa X ni budi kufungiwa haraka iwezekanavyo ili usiweze kuharibu vijana watato wengi pia kunapaswa kutengenezwa Sheria Kali ya Kudhibiti mapenzi ya jinsia moja na usagaji ili kusaidia kizazi kijacho kisiharibike.

"Mungu aliruhusu wanadamu wazaliane na wakaongezeke lakini hili tatizo hata siku moja haliwezi kuruhusu wanadamu wakazaliana na kuongezeka hivyo Mara moja mtandao wa X Ufungiwe,".

 

No comments