Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo wampongeza Rais Samia
Na Francis Peter, Dar es Salaam
Kuelekea mkutano wa JUMUIYA ya wafanyabiashira Kariakoo utakao fanyika juni 13 Dar es Salaam, wamemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuwawekea mazingira wezeshi ya ufanyabiashara ikiwemo namna ya utoaji mizigo bandarini
Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Juni 07/2024 Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashira Kariakoo Martini
Amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa kipaumbele kikubwa kwa wafanyabiashira ambapo wamekutana na wizara zaidia ya tano ikiwemo wizara ya fedha na wizara mama ya viwanda na biashara na kufanyamazungumzo yanayochangia uboreshaji wa mazingira ya biashara nchini.
Ameongeza kuwa katika kikao hicho kilichoongozwa na Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu kijaji aliwaahidi wafanyabiashira kuongeza bajeti ya wizara kwaajili ya kuboresha mazingira ya biashara,kuwakutanisha na TRA na kuweza kuangalia namna ya kupunguza utitiri wa kodi.
" Tumewaomba TRA wanapotekeleza majukumu yao wasijifiche,tushirikisha e ,tufanyekazi kwa pamoja tujenge nchi yetu sote, wafanyabiashira tupo tayari kulipa kodi bila shuruti, Nipende kutoa wito kwa TRA hata wanapoleta vijana wapya katika kukusanyakodi watutambulishe wasinifiche wakawa wanawawinda wafanyabiashira".
Aidha amebainisha baadhi ya Kero zinazoendelea wakabili wafanyabiashira hao kuwa ni pamoja na VAT,namna ya uwasilishaji wa risit za EFD, na uingizaji wa mizigo kutoka nje.
Wafanyabiashira wanaomba kodi zote ziishie bandarini na si kuwafwata mara kwa mara katika maeneo yao ya biashara ili kuepusha mianya ya rushwa
Post a Comment