BENKI YA AKIBA YATOA ELIMU YA FEDHA KWA WADAU MBALIMBALI
Na Mwandishi wetu
Benki ya Akiba imesema itaendelea kuunga mkono serikali kwa kutoa elimu ya fedha huku ikiboresha huduma zake nchi nzima ili kusaidia kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuchochea kukua kwa uchumi wa Taifa.
Ameyasema hayo Juni 14 ,2024 Jijini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Akiba Bw Silvest Arumasi wakati wa kuhitimisha mafunzo ya elimu ya fedha yaliyojumuisha viongozi wa benki hiyo ,watumishi kutoka Wizara , taasisi na ofisi mbalimbali za serikali lengo likiwa ni kubadilishana ujuzi na kujenga mahusiano mazuri huku wakifahamiana na kuweka mikakati ya pamoja namna ya kuwahudumia watumishi wa Umma kwa weledi zaidi na kujibu maswali na kujibu maswali huku wakitatua kero zinazojitokeza kiutendaji
Mkurugenzi Arumasi amebainisha kuwa benki hiyo itawaangalia wananchi wa Dodoma kwa upekee kutokana na fursa mpya zilizopo katika Jiji hilo kwani serikali imekuwa ikiendeleza na kustawisha Makao makuu ya Nchi hivyo ametoa rai kwa wananchi kujishughulisha na biashara na wanapokwama benki hiyo ipo kutoa mikopo kwa riba nafuu .
"Tunaahidi kuwa benki itaendelea kuunga mkono serikali kwa kuwasadia wananchi kuwapatia mikopo nafuuu ili kuinua mitaji yao pia kupanua wigo wa huduma nchi nzima ili kufikia azma ya kutoa mchango mkubwa wa kuwepo kwa huduma shirikishi za kifedha yaani financial inclusion" amesema Mkurugenzi Arumasi
Naye Bi Upendo Makula, Meneja wa Tawi la ACB - Dodoma aliwashukuru sana washiriki wote kwa kuitikia mwito kwa ujumla wao
Aidha washiriki wote waliishukuru Benki ya Akiba kwa mada nzuri za semina hiyo na wameahidi kutumia elimu hiyo kama chachu katika utendaji wao wa kila siku kwani wamejengewa msingi imara wa uelewa wa maswala ya fedha.
Post a Comment