DKT. MUCHUNGUZI: AMSHAURI MPINA SAKATA LA SUKARI KUSUBIRI UAMUZI WA SPIKA.
Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa na Kijamii Dkt. Dennis Muchunguzi amejitokeza mbele ya waandishi wa habari siku Chache baada ya Mbunge wa kisesa Luhaga Mpina kuzungumza na waandishi wa Habari juu ya la uagizaji wa sukari nchini.
Amesema amemshangaa Mbunge huyo kuzungumzia maelezo yake aliyoyapeleka kwa Spika juu ya sakata la uagizaji Sukari, kabla ya Spika na Bunge kutoa kauli.
Hivi karibuni Bungeni jijini Dodoma Mbunge wa Kisesa kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Luhaga Mpina aliibuka na hoja kuwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe na Serikali walikiuka Sheria ya uagizaji wa Sukari kupitia kampuni mbalimbali zikiwemo zilizosajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma za mawasiliano.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dkt. Muchunguzi amesema kwa kufanya hivyo maana yeka Mpina amefanya kosa kwani alitakiwa kusubiri majibu ya Spika Dkt. Tulia Ackson na Bunge kwa ujumla.
"Kama Mchunguzi sijamuelewa, nafikiri Mpina alipaswa kusubiri kauli ya Spika na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuzungumza mapema maana yake amem 'priemt' Spika, je inamaana hana Imani na Spika," amesema Dkt. Muchunguzi.
Dkt. Muchunguzi amesema kuwa kwa kuangalia lugha ya mwili alivyokuwa akizungumza Mpina inaonyesha kama ana mambo binafsi dhidi ya Bashe.
Kwamba kuhusu kampuni nyingine kama za simu kuagiza Sukari, amesema kuwa sio ajabu inapotokea dharuara kampuni inayofanya shughuli nyingine tofauti na kilimo, inaweza pia kuruhusiwa kuagiza ili kukabiliana na upungufu.
Amesema, kampuni hizo kupewa kibali cha kuagiza Sukari ilikuwa ni kwa nia njema.
"Hivyo unapokuwa kwenye Dharura ya upungufu wa Sukari inabidi utafakari ni namna gani unaweza kukabiliana na hali hiyo bila kukiuka Sheria," ameongeza Dkt. Muchunguzi.
Hata hivyo Dkt. Muchunguzi amewataka Watanzania kuwa watulivu juu ya Sakata hili huku wakisubiri kauli ya Spika Dkt. Tulia na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwamba suala hilo haliana haja ya kuwafawa wananchi, hivyo kauli ya Spika na Bunge ndiyo itakuja na majibu sahihi juu ya sakata hilo.
Post a Comment