Ads

RAIS EMBOLO KUPOKELEWA NA RAIS DKT. SAMIA IKULU DSM

Mheshimiwa Rais Embaló atapokelewa rasmi Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni 2024 na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Baada ya mapokezi hayo, viongozi hao watakuwa na mazungumzo ya faragha na baadaye watashiriki katika mazungumzo rasmi kuhusu uhusiano kati ya Tanzania na Guinea Bissau, na baadaye kuzungumza na Waandishi wa Habari kuelezea masuala muhimu yaliyojiri katika mazungumzo yao.

Sambamba na hayo Mheshimiwa Rais Embaló na ujumbe wake atatembelea Miundombinu ya Reli ya Kisasa katika Kituo cha Stesheni jijini Dar es Salaam, Mamlaka ya Eneo Huru la Uwekezaji kwa Mauzo Nje (EPZA) na taasisi ya Muungano wa Viongozi wa Afrika katika Kudhibiti Malaria (ALMA).


Ziara hiyo ni mwendelezo wa jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kuimarisha ushirikiano na nchi mbalimbali ili kuinufaisha nchi kiuchumi ikiwa ni utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi kwa vitendo.


No comments