Ads

TADB YAWAHIMIZA WAKAGUZI KUSHIRIKI MAJUKWAA ILI KUONGEZA UELEWA WA TEKNOLOJIA

BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imewahimiza wakaguzi wa ndani kutoka taasisi mbalimbali nchini kuendelea kushiriki katika majukwaa mbalimbali ili kujiongezea uelewa wa kina kuhusu utawala na teknolojia inayoathiri taaluma ya ukaguzi wa ndani.

Hayo ameyasema Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa TADB, Bi Joyce Maduhu katika kongamano la 10 la Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) lililofanyika jijini Arusha.

Kongamano hilo  la siku mbili limeandaliwa na Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani (IIA) Tanzania limelenga kuwaleta pamoja wataalamu wa ukaguzi wa ndani kutoka Afrika na sehemu nyingine za dunia.

Mwaka 2024, Tanzania imekuwa mwenyeji wa Mkutano wa Shirikisho la Taasisi za Ukagazi wa Ndani Afrika, (The African Federation of the lnstitutes of lnternal Auditors - AFIIA).

"Ili kukuza  taaluma ya ukaguzi wa ndani nchini, wito wangu ni kwamba, wakaguzi wote wanapaswa kushiriki mkutano huu ili kuendelea kunoa ujuzi na maarifa kulingana na kubadilika kwa haraka kwa teknologia na vihatarishi vyake vinayoathiri taaluma," alisema.

Mikutano kama hii ni fursa ya pekee kwa wakaguzi kuimarisha ujuzi wa kitaaluma, kupata ufahamu wa hali ya sasa na mwenendo wa tasnia, kujenga mtandao wa kitaalamu, na kupata fursa za ushirikiano na maendeleo ya kazi. Kwa hivyo, wakaguzi tunatarajia kuboresha ufanisi wa mifumo yao ya ukaguzi wa ndani na kuchangia katika maendeleo endelevu ya taaluma, ameongeza Bi. Maduhu.

Akitoa mwanga kwenye kongamano hilo, Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani (IIA) Tanzania Dkt. Zelia Njeza amesema washiriki wapatao 350 kutoka nchi 27 za ndani na nje ya Bara la Afrika, wanatarajiwa kushiriki kongamano hilo.

"Takriban Wakaguzi wa Ndani 1000 wanashiriki katika kongamano la mwaka huu," alisema.

Dkt. Njeza amesema pia kongamano la mwaka huu lenye mada ya ‘Beyond Boundaries Make Difference’ linalenga kuleta matokeo chanya, kuvunja mipaka, kuvuka vikwazo na kwenda juu zaidi. 

Nakuongeza kuwa "Inatia moyo kwa wataaluma wa ukaguzi wa ndani, watu binafsi au vikundi kufikiria kwa njia mpya na kutenda kwa njia zinazopita vizuizi na matarajio ya kawaida."

Hivi karibuni, TADB ilisaini mkataba mpya na Benki ya Biashara Tanzania (TCB) ili kuongeza dhamana ya mikopo kwa wakulima wadogo kupitia Mfuko Wadhamana wa Wakulima Wadogo (SCGS)

TADB imesema mkataba mpya wa miaka mitano wa ushirikiano na TCB uliosainiwa jijini Dar es Salaam ulikuwa na thamani ya shilingi bilioni 21 kutoka bilioni 7 za mkataba wa awali wa mwaka 2018 wakati Mfuko wa Dhamana wa Wakulima Wadogo ulipoanzishwa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mwendeshaaji wa TADB, Bw. Frank Nyabundege alisema makubaliano yaliyotekelezwa kupitia SCGS yataongeza upatikanaji wa mikopo kwa wakulima wadogo maradufu tofauti na hapo awali.





No comments