Ads

Benk ya ACB yazindua Rasmi huduma ya Kadi za VISA

Na Francisco Peter

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ,Silvest Arumasi amesema kwamba  Benki ya Akiba (ACB )  inafanya maboresho makubwa ya huduma za kifedha kwa wateja wake ili kuendana na mahitaji  ya soko.

Benki ya Akiba (ACB) katika maboresho hayo imezindua rasmi huduma ya kadi za VISA ambazo ni mahususi kwa kufanya huduma za miala ya kifedha  ambapo inauwezo wa kutumika sehemu yoyote Duniani.

Aidha amesema kwamba maboreshao hayo yatasaidia  kukidhi matarajio ya wateja ambapo hivi sasa huduma nyingi za kibenki zinatolewa kidigitali nakusaidia wateja kupata huduma kwa haraka na rahisi zaidi.

"Huduma za ACB VISA CARD zinamrahisishia mteja kufanya miamala mbalimbali kidigitali mfano ;  kutoa pesa kwenye ATM mbalimbali za VISA popote Duniani, na kufanya manunuzi mtandaoni, kufanya malipo kwenye vituo vya mafuta, kwenye migahawa na kwenye maduka makubwa ( Shopping malls & supermarkets) na nyingine nyingi" amesema Silvest

Bw. Silvest amewashukuru wateja wote kwa kuendelea kuiamini ACB na kufanya biashara kupitia benki hiyo, nakuwaomba Wajasiriamali na Wafanyakazi kutoka taasisi za umma na binafsi kujiunga na benki ya ACB ili kufurahia huduma bora zaidi kwa uharaka, unafuu na usalama



No comments