Ads

Namoto : Mpaka sasa KAWASO kimepata mafanikio makubwa licha ya baadhi ya watu wanaobeza mafanikio hayo.

Viongozi ambao watachaguliwa  hivi karibuni utakapo tangazwa  ambapo kwa sasa mchakato wa maandalizi unaendelea, 2024 ,wawe ambao kauli yao ya pamoja ni kutengeneza kariakoo ya pamoja,kariakoo ya upendo,Mshikamano,na kufikia ndoto za maendeleo.


Uchaguzi wa Viongozi wa KAWASO utafanyika April 19 , 2024 huku akiwasisitiza wanachama kuchagua viongozi wenye maono ya kukifikisha mbali chama hicho.

Akizungumza kuelekea uchaguzi huo Mwenyekiti wa KAWASO Namoto Yusuph Namoto amesema mpaka sasa Chama hicho kimepata mafanikio makubwa licha ya baadhi ya watu wanaobeza mafanikio hayo.

"KAWASO imefanikiwa katika mambo mbalimbali ikiwemo kuondoa migogoro kati ya Machinga na uongozi wa halmashauri ya wilaya, kua na kanzi data ya kuwatambua wamachinga, kupata vitambulisho vya NIDA na TRA , kupata mikopo ya mitaji na viwanja kutoka taasisi za kifedha ikiwemo Benki ya Maendeleo, pamoja na kuhakikisha utunzaji wa mazingira unatekelezwa ipasavyo,"amesema Namoto.

Katika hatua nyingine Namoto amewasisitiza wamachinga kumuunga mkono rais Dkt Samia Suluhu Hassan kulinda amani na kuacha kutumika na watu wenye nia ovu ya kuvunja amani ya Taifa la Tanzania ambalo linasifika kwa tunu za Amani, Mshikamano na Upendo.

No comments