Ads

Alex Masawe wa Kata ya Ndugumbi atoa madawati 150 Shule ya Sekondari Turiani Magomeni

Diwani wa kata ya Ndugumbi  iliyopo wilaya ya kinondoni maeneo ya magomeni kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Alex Masawe amesema anaishukuru serikali kwa kutoa meza na viti 150 kwenyeshule ya sekondari Turiani.

Hayo yamesemwa jiji  Dar es Salaam na Masawe alipokuwa akikabidhi meza na viti katika shule hiyo ambapo  amehimiza wanafunzi  wa shule hiyo kusoma kwa bidii.

"Napenda kuona ufaulu wenu unakuwa mzuri zaidi kwani hatua hii ya kuwalete meza na viti naamini itazidi kukuza hamasa juu ya kusoma masomo yenu," alisema Masawe.

Aliongeza kusema  kuwa jamii yote iliyopata elimu bora ni msaada kwa Taifa letu na pia ni msaada kwa familiya za kitanzania.

Kwa upanda wake mwalimu Mkuu wa shule hiyo Janet Mabusa ameipongeza serikali kwa hatua hiyo kupata meza na viti vya kusomea wanafunzi kwa kuwa vitachochea wanafunzi kusoma na kuongeza ufaulu mzuri.

Janet aliendelea kupongeza uongozi wa diwani Masawe kwa hatua yake ya kuleta meza na viti .

"Niliomba matawati 200 lakini nashukuru kupata meza na viti 150 kwa kuwa vitasaidia kuondoa changamoto ya uhaba wa wanafunzi kukosa madawati,"amesema Janet.

Kwa upande wake mwanafunzi Rosemery Jemes anayesoma kidatu cha kwanza amesema kuwa hali ya kupokea msaada huo utachangia ufaulu wao kuwa juu.




No comments