EFM YABUNI MBINU MPYA KUFIKA FURSA KWA VIJANA
Na Francis Peter, Dar es Salaam
Kituo cha Redio cha EFM imebuni mbinu mpya ya kuwafika kundi kubwa la vijana kuzifika fursa kwa kuleta "Kitaa Hub".
Hatua hiyo imekuja baada ya kutimiza miaka 10 tangua kuanzishwa kwa kituo cha redio cha EFM ikiwa na lengo kufikia kundi kubwa la Vijana.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Francis Sizza maarufu kama Majizzo amesema
kupitia EFM atatimiza maono yake ya kuwainua vijana kupitia kampeni ya Majizzo
Jobs Campaign.
Aidha amesema jukwaa la Kitaa Hub litakuwa
jukwaa mahususi lenye lengo la kuwapa vijana nafasi ya kujifunza, kukua na hata
kushindana katika soko la ndani na kimataifa.
“ Lengo letu ni kufikia kundi kubwa la vijana
kwenye field tofauti tofauti, naongelea vinyozi, fundi uashi, wapishi, wasusi,
dada wa kazi, madereva, wasanii, waandishi wa nyimbo, DJS na graduates na
wengine wengi Kwa kifupi ni uwanja wa kujidai onyesha uwezo wako” Amesema
Majjizo.
Kwa upande wake mjumbe wa timu inayosimamia
jukwaa hilo Dkt Albert Komba amesema kwamba jukwaa la Kitaa hubs litasaidia
kuwajengea uwezo vijana wanaotafuta ajira na kuwaunganisha na waajiri Kwa
urahisi zaidi.
Aidha amesema kwa sasa kiwango Cha ajira
chini kipo chini hivyo serikali na taasisi binafsi hazina budi kushirikiana
kutafuta mwarobaini wa tatizo Hilo nakisusisitiza kuwa kupitia Kitaa hubs
intasiadia kupunguza tatizo la ajira Kwa vijana ambao Wana vipaji vya aina
mbalimbali.
“Hili jukwaa la Kitaa hubs pamoja na Majizzo
jobs Compaign itaweza kukutanisha vijana nchi nzima ili kuweza kuonyesha vipaji
vyao,naamini kuanzishwa kwa jukwaa hili itasaidia vijana kutoa mawazo
yao,bunifu zao na kuweza kufikia ndoto zao Kwa urahisi zaidi” amesema Dkt
Komba.
Hata hivyo vijana waliojitokeza katika
mkutano huo wamepongeza kuanzishwa kwa jukwaa la Kitaa hubs kwani litawasaidia
kuwasimamia katika kupata kazi nzuri na zenye staha huku wakisisitiza kuwepo
Kwa usalama wa taarifa zao kwenye mtandao huo wa website.
Post a Comment