Ads

TANZANIA NA HUNGARY ZASAINI MAKUBALINAO YA USHIRIKIANO YENYE KULETA TIJA KWA TAIFA

Francisco Peter

TANZANIA na Hungary zimesain makubaliano ya kushirikiana katika masuala ya maji pamoja huku ikielezwa kuwa Hungary hivi karibuni wanatarajiwa kufungua ubaloya nchini Tanzania. 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Machi 24, 2024 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Januari Makamba, amesema kuwa wamepata ugeni kutoka Hungary baaada  ya Rais wao kuja Tanzania mwaka jana kwa ajili ya  kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu uliopo baina ya nchini zetu mbili.
Amesema  kuwa katika mazungumzo hayo baina yao na ujumbe wa Hungary ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje  wa taifa hilo, Peter Szijjàrtò wamekubaliana mambo mengi ikiwemo kuanzisha safari za anga ya moja kwa moja hadi hapa nchini.

Waziri Makamba amefafanua kuwa safari za anga ya moja kwa moja kutoka Hungary kuja Tanzania itasaidia kutanua wigo  wa kibiashara baina ya mataifa hayo mawili.

Pia itaongeza watalii wanaotoka Hungary kuja Tanzania ambapo kwa miaka miwili iliyopita watalii 5000 waliingia hapa nchini kutoka katika nchi hiyo na mwaka jana waliongezeka na kufikia 11,000.

Kulingana na ongezeko hilo la watalii wanaotoka Hungary kuja Tanzania kuongezeka anaamini kuwa pindi itakapoanzishwa safari hiyo ya anga wataongezeka na kufungua fursa nyingi za kibiashara.

Katika nyanja ya kibiashara wamekubaliana kwa pamoja  kuandaa makongamano ya sekta binafsi watakaokwenda ziara Hungary na wataifa hili kuja Tanzania.

Pia wamekubaliana kuendeleza  ushiriano kwenye elimu na kuongeza scholarship kwa Watanzania kwenda kusoma Hungary na Tanzania itakuwa ikitoa nafasi tano kwa vijana wa nchi hiyo kuja kusoma hapa nchini katika vyuo mbalimbali vilivyopo kila mwaka.

"Hadi sasa tayari wanafunzi 146 wa kitanzania wamepata fursa ya kusoma nchini Hungary na kila mwaka tunapeleka vijana wetu kusoma huko na hiyo imekuja baada ya wenzetu mwaka 2018 kuanzisha programu ya Scholarship   amesema.

Akifafanua sababu ya kusainj mkataba wa kushirikiana katika sekta ya maji asema sababu ya kuchukua hatua hiyo ni kutokana na taifa hilo kuwa kuongoza katika teknolojia ya kudhibiti mafuliko, maji taka na ya kutumia.

Maarifa yao makubwa katika sekta ya maji ndio imetuvutia kusaini mkataba unaohusu masuala hayo ili nasi tupate utaalamu wa kutosha katika nyanja hiyo, amesema

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungary, Peter amesema kusaini mkataba huo na usafri wa anga utasaidia kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya mataifa hayo mawili.




No comments