Ads

DKT. MAHELA AWATAKA MAKATIBU KUSIMAMIA FEDHA ZA CHANJO ILI KULETA TIJA KWA TAIFA

Na Francisco Peter, Dar es Salaam.

Waratibu wa Afya ngazi zote wametakiwa kuhakikisha wanasimamia fedha za chanjo na lishe zinazotolewa na Wadau pamoja na Serikali zinafika zinapokusudiwa kwa wakati ili kupunguza tatizo la Ukosefu wa elimu ya lishe na magonjwa ya mlipuko.

Maelekezo hayo yametolewa Februari 3,2024 na Naibu katibu Mkuu OR-Tamisemi anayeshughulikia Afya Dkt. Dkt Charles Mahela jijini Dar es Salam Wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa tathimini ya huduma za chanjo nchini kwa mwaka 2023 ambapo amewasisitiza Wasimamizi kutosita kuwachukulia hatua  wale wote watakao bainika wamehusika na ubadhilifu wa fedha hizo.

“Ushirikiano hafifu, kukosa mipango na mikakati pamoja na Matumizi Mabaya ya fedha vimekua changamoto ya kukwamisha huduma bora za lishe na chanjo, Tumekuwa tukipokea fedha kutoka shirika la GAVI kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za Chanjo.

"Hata hivyo suala hili halijapewa kipaumbele, hivyo niwakumbushe tena kila Mkoa ukusanye nyaraka hizo na kuziwasilisha OR-TAMISEMI kabla ya tarehe 15 Februari 2024 kwa ajili ya hatua nyingine” amesisitiza  Dkt. Charles.

Dkt. Charles ameendelea kusema kuwa  kila Mkoa ni vema uimarishe ufuatiliaji na tathmini za utekelezaji wa Mkakati wa Kumfikia Mtoto kwa Chanjo (Reach Every Child) katika ngazi ya vituo vyote  vya huduma za Afya.

“Mikoa na Halmashauri ziimarishe usimamizi na kutoa Msaada wa kiufundi kwenye vituo vya huduma ili kuinua kiwango cha ubora wa huduma zinazotolewa. OR-TAMISEMI kwa kushirkiana na Wizara ya Afya itaendelea kutafuta rasilimali kadiri fursa zinavyopatikana na kuzielekeza rasilimali hizo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kuimarisha huduma za Afya Msingi ikiwemo Chanjo,” amesema Dkt. Charles.

Kuelekea utekelezaji wa Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya Surua na Rubella inayotarajiwa kuanza tarehe 15 hadi 18 Februari, 2024, Dkt. Charles amesisistiza wasimamizi wa kampeni hio kuhakikisha Watoto wote wanafikiwa pamoja fedha zilizotengwa kwa shughuli hiyo zinatumika vizuri


No comments