Serikali yaonya Wafanyabiashara ya Sukari Wanaojipangia Bei Kuwaumiza Wananchi nchini
Serikali nchini imesema hakuna sababu yeyote , wafanya biashara kujipangia bei kwa kutumia uhaba wa sukari kujipangia bei hali inayopelekea kuwaumiza wananchi.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) Prof. Kenneth Bengesi wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema ni kweli Kuna changamoto ya uhaba wa sukari lakini wasitumie njia hiyo kuwauzia wananchi mara mbili au tatu ya bei ya kawaida.
“Tunashangaa kusikia kuwa bei ya sukari imepanda kutoka bei ya kawaida ya shilingi 3000 hadi 6000 niwatake wafanyabiashara waache mchezo huo kwani sukari wananunua kwa bei Ile Ile “Amesema Prof. Bengesi.t
Hata hivyo amesema hatua nyingine ni serikali kutoa kibali cha kuagiza sukari toka nje ya nchi kiasi cha Tani elfu 50 ambapo itaanza kuingia nchini kuanzia Januari 22 hivyo uhaba wa sukari utapungua.
Sambamba na hayo amesema uhitaji wa sukari nchini ni Tani laki Tano na ishirini (50020) na Viwanda vinauwezo wa kuzalisha Tani laki Tano na arobaini na Tano (500045).
Post a Comment