Ads

DCEA YAWAKAMATA WATU SABA KWA KUHUMA ZA KUUZA DAWA ZA KULEVYA

Na Francisco Peter

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa Kulevya nchini (DCEA)imesema imekamata jumla ya watu saba  ambapo wawili kati yao wana asiliya Asia nakuwa watuhumiwa waliokamatwa ni miongoni mwa mitandao mikubwa ya wauzaji wa dawa za kulevya inayofuatiliwa nchini na duniani.



Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Kamishna Jeneralwa DCEA Aretas Lyimo amesema kuwaimeweza kukamata kiasi kikubwa  cha dawa za kulevya ambacho hakijawai kukamatwa katika historia ya Tanzania tangu kuanzakwa shughuli za udhibiti wa dawa za kulevya huku jumla ya kilogram 3182 za dawa za kulevya aina ya Heroin na Methamphetamine katika oparesheni hiyo maalum iliyofanyikajijini Dar es Salaam na Iringa kati ya tarehe 5 hadi 23  Dicemba mwaka 2023 zikikamatwa.

"Kiasi hiki ha dawa za kulevya kinajumuisha kilogramu 2,180,29 za dawa aina ya methamphetamine na kilogramu 1001.71 aina ya heroin zilizokamatwa katika wilaya za kigamboni, ubungo na kinondoni jijini Dar es Salaam pamoja na Wilaya ya Iringa mkoani Inringa"amesema Kamishna Lyimo.

Aidha, dawa hizo zilizokamatwa zilikuwa zimefungashwa kwenye vifungashio zenye chapa mbalimbali za kahawa na majaninya chai ambapo mbinu hiyo inatumika kwa lengo labusafirishaji wake na kukwepa kubainika

Hata hivyo, amesema kuwa dawa aina ya methamphetamine ni dawa mpya ya kulevya iliyopo katika kundi la vichangamshi sawa cocaine ambapo dawa hiyo huwa kwenye mfumo wa vidonge, unga au chembembe mithili ya chunvi ang'avu yenye rangi mbalimbali ambayo huzalishwa kwenye maabara bubukwa kuchanganya aina mbalimbali za kemikali bashirifu

"Dawa hii ni hatari kwa afya ya mtumiaji madhara yake ni makubwa na hayatibiki kirahisi kwani mtumiaji hupata madhara ya kudumu kwenye ubongo na hivyo hupunguza uwezo wa kutunza kumbukumbu kusababisha uraibu na kuathiri mfumo mzima wa fahamu.

Ameongeza kuwa, kiasi cha dawa za kulevya zilizokamatwa zingefanikiwa kuingia mtaani zingeweza kuathiri zaid ya watu 76, 368,000 kwa siku hivyo, ukamataji huo umeokoa nguvu kazi ambayo ingeangamia kutokana na madhara yatokanayo na madawa ya kulevya ndani na nje ya nchi.

Sambamba na hayo DCEA imetoa onyo kwa wote wanaoendelea kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya nchini Tanzania badala yake wajikite kwenye biashara nyengine halali kwani mamlaka imejidhatiti kukomesha biashara hiyo kwa kufabya oparesheni katika maeneo mbalimbali nchin.

Aidha, DCEA imeishukuru Serikali ya Jamuhuri ya muunganobwa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluh Hassa kwa kuendelea kuiwezesha mamlaka hiyo katika kutekeleza kazibzake kwa ufanisi mkubwa.

No comments