Ads

CCM YAWATAKA WANANCHI KUSHIRIKI MAONI DIRA YA TAIFA.


 
Na John Luhende
Chama Cha Mapinduzi CCM  kimewataka wananchi kushiriki kikamilifu kutoa maoni yao kuhusu mabadiliko  ya Sheria na dira ya Taifa.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa NEC itikadi na uenezi wa chama Cha mapinduzi Paul Makonda Leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishinwa habari .

Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua na kutoa fursa kwa Watanzanja wote kutoa maoni katika hili, wataalamu, Wafanyabiashara, Wasomi, Mafundi ujenzi na Watu wotee yani kila Mwananchi ana wajibu wa kushiriki kutoa maoni ya kutaka kuona Tanzania inatakiwa kuwa ya namna gani"

Pia  chama hicho kimetoa Rai kwa wananchi wote  kwamba majimbo na kata bado vinauongozi kwa hiyo wasianze kujiingiza Katika Katika kutafuta kuungwa mkono kwa kutoa michango mbalimbali.  

Aidha CCM  kimetoarai kwa watu walio na shauku ya kutaka Majimbo na Udiwani, sasa CCM inasema chokochoko zote ziachwe mara moja, wabunge wapewe nafasi ya kufanya kazi zao kama ulivyo utaratibu na katika hili nitoe mfano mimi niligombea ubunge Kigamboni nikashindwa na akateuliwa mgombea wa Chama kwa kura za maoni na mimi nikakubali kushindwa na kuacha na sijawahi tena kwenda kigamboni nimemuacha mbunge afanye kazi zake"

"Acheni kuwanyima utulivu viongozi wetu, waacheni wafanye kazi zao, acheni kuwachafua huko kwenye magroups ya whatsapp, tuwape ushirikiano kwasababu kumuyumbisha maana yake unayumbisha utekelezaji wa Ilani ya CCM, Marufuku kufanya hivyo"

No comments