Ads

RC CHALAMILA AKESHA MVUA ILIVYOHARIBU MIUNDOMBINU YA BARABARA

NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila anafanya ziara  ya kukagua ujenzi wa barabara, madaraja yaliyoharibiwa na mvua ili kuhakikisha wananchi wanapita katika maeneo hayo haraka iwezekanavyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuendelea kutabiri uwepo mvua kubwa katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na kutoa tahadhari kwa wananchi na sekta mbalimbali kuchukua hatua kwa ajili ya kukabiliana ma madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo kuharibufu wa miundombinu ya barabara.

Akiwa katika Daraja la Mbopo lililokuwa limekatika Mhe. Mkuu wa Mkoa amekuta hatua za haraka zimeshachukuliwa, huku akitoa maagizo kwa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuwa ifikapo saa tano ya leo daraja hilo Liwe linapitika ili kuondoa usumbufu kwa wananchi.

Pia RC Chalamila alipofika katika Daraja la Tanganyika alikuta Daraja hilo limeathirika kutokana na mabadiliko ya mto kuhama na kwenda katika makazi ya watu.

RC Chalamila ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuendelea kufatilia taarifa za TMA pamoja na kuchukua tahadhari.

Kwa upande wake Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Geofrey Mkinga amekili kupokea maagizo yote na kuahidi kuyafanyia kazi.

No comments