Ads

WAZIRI DKT. NDUMBARO ATOA MAAGIZO BMT KUHAKIKISHA WACHEZAJI WAMEKATIWA BIMA YA AFYA

Na Francisco Peter

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro ameliagiza Baraza la Michezo la Taifa( BMT) kuhakikisha mwezi January 2024 Wachezaji wa Vilabu vyote vinavyoshiriki  Ligi Kuuu Tanzania Bara wawe wamekatiwa huduma ya bima hali itakayochangia kuongezeka kwa idadi ya watu wanaopata huduma hiyo.


Dkt. Ndumbaro ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) ishirikiane na wadau wa bima ili  kulinda haki za watumiaji wa huduma za bima nakuifanya sekta hiyo  iaminike nakua kimbilio la wananchi wote.

 

Amesema Bima katika Michezo ni eneo muhimu na nipana zaidi kwasababu kuna wadau wengi,TIRA mnaweza kulitumia eneo hili nakuweza kupata watumiaji wengi wa bidhaa zenu,napenda kutumia fursa hii kuiagiza BMT kuanzia January mosi mwakani, timu zote za zinazo shirika ligi kuu ya NBC  wachezaji wote wawe na bima kuna fursa zaidi kwa watu wa bima kwa upande wa michezo" amesema.


Waziri Dkta Ndumbaro ametoa maagizo hayo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Nchemba  Disemba 6 jijini Dar es Salaam wakati akimwakilisha kwenye  uzinduzi wa taarifa ya utendaji wa soko la bima kwa mwaka 2022 uliohudhuliwa na wadau mbalimbali wa bima Nchini.

 

“Naomba muendelee kutoa elimu ya umuhimu wa Bima na bidhaa zake kwa wananchi ,muwafikiwe watu wengi waliopo vijijini na mjini ambapo watanzania wengi wanawahitaji hasa huduma ya bima ,bima ya afya kwa wote ni haki ya kila mtu apate huduma sawa awe tajiri au masikini,amesisitiza Dk. Ndumbaro.

 

Waziri huyo wa Utamaduni,Sanaa na Michezo ameipongeza TIRA kwa kuzingatia mambo muhimu matatu wakati wa uandaaji wa taarifa hiyo ikiwemo kujenga uelewa mpana kwenye bidhaa zake na umuhimu wake nakwamba kwasasa bado uelewa ni mdogo hivyo wadau wote washirikiane kuwaelimisha wananchi.

 

“Kazi ya bima ni kulinda mali na maisha ya watu , wadau wa bima mshirikiane na TIRA muweka vifurushi(Package )za aina mbalimbali kuwezesha kila mwananchi aweze kumudu huduma za bima,” amesema.

 

Ameongeza kuwa TIRA kwa kushirikiana na wadau iweke mikakati ya kutoa huduma ya bima kidigital na kuhakikisha inasimamia wananchi wapate  huduma stahiki na kudhibiti ubadhilifu ili kuwezesha pia kukuza pato la taifa.


 

Naye Kamishina wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) Dk. Baghayo Saqware amesema Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ametia saini mswaada wa sheria ya bima ya afya kwa wote na sasa imekuwa sheria kamili wapo tayari kusimamia biashara ya bima na kufanya kazi nchini.

 

Kamishna Saqware amesema hadi kufikia Disemba 31 mwaka 2022 jumla ya kampuni 36 ni za bima,nakwamba hadi sasa kampuni zaidi zinaongezeka na wakala wa bima mwaka 2021 walikua ni 789 huku meaka 2022 wakifikia idadi ya 922.

 

“Mwaka 2022 ilipokea malalamiko 332 ambapo kampuni ya Insurance Group Tanzania limited ikiongoza kwa malalamiko 82 sawa na asilimia 59.0 na kampuni zingine, “amesema Kamishina Dk.Saqware.

 

Aidha Kamishna huyo wa TIRA amezitaja nchi ambazo zinafanya kazi na soko la bima nchini kuwa ni pamoja na Kenya, Afrika Kusini, India na Uingereza ambapo  soko hilo linachangia uchumi kwa asilimia kubwa hapa Nchini Tanzania.

No comments