Ads

BETIKA NA TIGO WAZINDUA KAMPENI YA TWENZETU IVORY - COAST Ki-VIP

Na Francisco Peter

KUELEKEA Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yanayotarajiwa kuanza January 13 2024 Jijini Abdjan Ivory Coast Kampuni ya Kubashiri Tanzania Betika kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tigo imezindua Kampeni kubwa ya "Twenzetu Ivory -Coast Ki-VIP" .

Akizungumza leo Desemba 6, 2023 Jijini Dar es salaam Afisa Habari Betika Tanzania Rugambwa Juvenalius amesema Kampeni hiyo ni kwa ajili ya wateja wa Betika wanaotumia Mtandao wa Tigo hivyo wanaendelea kuwajali kwa kuwapa huduma bora ambapo promotion hiyo nzuri itaambatana na zawadi za kutosha kwa watanzania kuanzia msimu huu wa sikukuu mpaka Michuano yenyewe.

"Tembelea tovuti ya Betika www.betika .co.tz vilevile unaweza kuingia kwenye drop kwa kubeti kupitia huduma y SMS tuma neno BETIK kwenda 15316 sambamba na hilo unaweza kubeti kwenye menyu ya kupiga *149*16# weka pesa kwenye akaunti yako ya Betika kwa kutumia Tigo pesa na ufanye ubashiri kila siku ili uweze kujishindia zawadi kibao na kupata fursa ya kushuhudia Michuano mikubwa wa soka barano Afrika"amesema Rugambwa.

Hata hivyo amesema Mabongwa watapatikna kwa njia ya droo za kila siku na droo kubwa ya wiki itakuwa kila jumatatu wadau wanachotakiwa ni kubashiri mechi  mbalimbali kila siku na mabingwa wa droo ya wiki watatangazwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram na Facebook.

Rugambwa amesema Droo kubwa ya kupata Mabingwa 6 watakaoenda  Ivory Coast itanyika January 1, 2024  na Mabingwa hao watapata huduma za Ki-VIP kuanzia wakiwa Tanzania mpaka kufika Ivory Coast ambapo watapatiwa tiketi za ndegw kwenda na kurudi ,hoteli kwa siku zote Ivory Coast na usafiri wa kifahari kuelekea uwanjani na tiketi za kutazama mechi Uwanjani, hivyo wateja wote mnakaribishwa  kutumia fursa hiyo.

Naye Meneja Biashara Tigo Pesa Fabian Felician amebainisha kuwa promotion hiyo itakuwa pia na zawadi ikiwemo TV Hisense yenye nchi 70  kila wiki kwa washindi wawili zikiambatana na Ving'amuzi vya DStv na kifurushi cha mwezi mmoja hivyo mamilioni kushindaniwa kwenye droo za kila siku na zawadi kubwa nono.

No comments