Ads

SERIKALI KUBORESHA SHERIA KUNUSURU VIWANDA VYA KUTENGENEZA MAGARI NCHINI

Na Francisco Peter

SERIKALI imesema ipo mbioni kuifanyia marekebisho sheria ya uagizaji magari nchini ambayo inaruhusu hadi magari chakavu kuingia nchini ili kuzuia magari hayo kusaidia kunusuru viwanda vya utengenezaji magari nchini.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji,Profesa Kitila Mkumbo,wakati wa uzinduzi wa Magari ya MAHINDRA yaliotengenezwa kwa ubia Baina ya kiwanda G truck na Mahindra ya nchini India.

Aidha, Profesa Mkumbo,amesema l kwa sasa hapa nchini kumekuwa na viwanda vinavyotengeneza magari hivyo ni wakati wa kubadilisha sheria ya uigizaji magari.

“Sheria ya sasa inaruhusu mpaka magari chakavu yaingie nchini hivyo sheria tutaibadilishe ili kulinda viwanda hivi vinavyozalisha magari hapa nchini”Amesema Profesa Mkumbo.

Hata hivyo,Profesa Mkumbo amesema ujio wa kampuni ya Mahindra ni matokeo ya ziara ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania aliyoifanya nchini India mwezi Octoba mwaka huu.

No comments