Ads

MVUA YAANGUSHA NYUMBA 51 SHINYANGA

Wananchi wa Kijiji Cha Ibanza Kata ya Mwamala Wilaya ya Shinyanga wanaishi katika mazingira magumu baada ya  Nyumba zao kuanguka kufatia mvua kubwa zilizoambatana na upepo mkali  kunyesha usiku wa kuamkia Disemba 6, 2023 majira ya saa 9 usiku.

Mvua hizo na upepo mkali zimevunja Nyumba 51 na  kusababisha wananchi kukosa makazi pamoja na kuathiri mashamba na mifugo.

Kufatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amefika eneo tukio na kutoa pole kwa waathirika  wa mvua hizo, huku akibainisha kuwa Serikali ipo pamoja nao katika kipindi hiki ikiwemo kugharamia matibabu wananchi ambao wamepata majehara.

Mndeme amesema kuwa mbali na kugharamia matibabu, pia wananchi ambao mashamba yao yameharibika watapewa mbegu bure ili wapande upya kwa sababu mvua bado zinaendelea kunyesha. 

"Wale ambao watahitaji Maturubai watapewa, nawapongeza wananchi ambao wamejitolea kuwahifadhi ndugu zao kwa muda" amesema Mndeme.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Simon Berege, amesema kuwa mvu hizo zimeharibu mashamba ya mahindi hekari 10,  kuku 20 na mbuzi mmoja wamekufa.

"Hkuna kifo cha mtu yoyote na Bibi ambaye amevunjika Mguu anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga" amesema Berege.

Mmoja wa waathirika wa tukio hilo Jilala Dutu, amesema mvua ilianza kunyesha majira hayo ya usiku huku wakiwa wamelala, lakini ghafla walisikia mabati yakibebwa na upepo na kutupwa pembeni na nyumba yao.







Hata hivyo kwa mujibu utabiri wa Hali ya Hewa unaotolewa  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Disemba 6, 2023 imetoa angalizo la mvua kubwa katika baadhi ya Mikoa ikiwemo Rukwa, Shinyanga, Njombe, Songwe, Tabora, pamoja Mbeya.

No comments