Ads

RAIS DKT. SAMIA KUFUNGUA MKUTANO KITAIFA DIRA YA MAENDELEO

Na Francisco Peter

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua Mkutano wa kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Maendeleo ya Taifa Desemba 9/2023 ambapo pato la taifa la mtanzania limeongezeka hadi Dola za kimarekani 1200 (TZS 2,880,000).



Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Mipango na uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema kuwa Mkutano huo unalenga kupokea na kujadili taarifa ya kitafiti ya Tathimini ya Utekelezaji wa Dira ya Maendeleo 2025 ambayo inaonyesha kuwa pato la mtanzania limeongezeka kutoka Dola za kimarekani 399.5(TZS 322,597) mwaka 2000 hadi kufikia Dola 1200(TZS 2,880,000) mwaka 2022.

” Lengo kuu la mkutano huu ni kuzindua, kupokea na kujadili taarifa ya kitafiti ya tathimini ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na kuainisha mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa Dira ya mwaka ya Taifa ya Maendeleo” Amesema Prof.Mkumbo.

Aidha amesema Tanzania imefikia Asilimia 124 ya kujitosheleza kwa chakula ikilinganishwa na lengo la asilimia 140 ifikapo 2025 ambapo hatua hiyo imewezesha Tanzania kukabiliana na njaa kwa mikoa na Wilaya zote nchini.

“Mtandao wa Barabara za lami na zege katika Mikoa umeonfezeka kutoka kilometa kilometa 4,179 kwa Mwaka 2000 hadi kufikia kilometa11,966.38 mwaka huu”Aliongeza Profesa kitilya Mkumbo.
Professa Kitilya Alisisitiza kuwa Vifo vya uzazi vimepungua kutoka Vifo 760 hadi kufikia 104 kwa mwaka 2022.

Katika mkutano huo pia Rais atazindua rasmi timu kuu ya kitaalam ya Dira (National Vision Core Technical Team) na kamati ya usimamizi wa Dira ( National Vision Steering Committee) pamoja na nyenzo za kidigitali zitakazotumika katika kukusanya maoni ya wadau.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Mtendaji wa Tume ya Mipango Laurance Mafuru amesema kuwa lengo Mpango wa pili wa Maendeleo 2025 unalenga kupunguza umasikini na kuongeza Ajira.

Amesema Mpango huo unaotarajiwa kuzinduliwa Desemba 9 Mwaka huu na Rais Dk Samia Suluhu 

Hassan unalenga ujenzi wa Miundombinu sambamba ukuaji wa uchumi na mkakati wa kuboresha Sekta ya viwanda, kilimo na uboreshwaji wa Huduma ikiwemo Maji na Elimu.

No comments