Ads

DIWANI KATA YA TABATA YA KIMANGA ALIVYOTEKELEZA ILANI YA CCM

Na Francisco Peter

DIWANI wa Kata ya Tabata Kimanga, Patory Kiombya amesema Kata hiyo inaenda kufunguka kimiundombinu kwakuwa Barabara za mitaa sita katika kata hiyo zitajengwa kwa kiwango cha lami.

Kiwombya aliyasema hayo alipozungumza na sikuchache zilizopita ofisini kwake Tabata Kimanga jana ambapo gazeti hili lilitaka kufahamu utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi wa 2020/2025 umefanikiwa kwa kiasi gani.

“Ni mengi tumefanya kwa nafasi yetu kama chama na serikali lakini kubwa zaidi katika Mradi wa Uendelezaji jiji la Dar es Salaam (DMDP) awamu ya pili Tabata inakwenda kufunguka kimiundombinu hususani ujenzi wa Barabara na vivuko vyake” alisema

Alisema kwa sasa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inafanya tathimini zake kuhusu Barabara hizo na ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Ilala imekwisha tenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Barabara hizo ambapo baada ya tathimini hiyo itajulikana zitagharimu kiasi gani cha fedha.

Aidha amesema na ujenzi wa Barabara hizo sita kwa kiwango cha lami, kuna urekibishwaji wa magleda katika halmashauri ya Ilala yapatayo matatu na muda wowote kuanzia sasa yatakapotengenezwa yatatumika pia katika utengenezaji wa Barabara za mitaa ya kata hiyo kwa kiwangu cha changarawe pamoja na ujenzi wa vivuko viwili kikiwemo kinachonunganisha Tanbata Kimnga na kwa Manyaunyau na Kimanga Mawenzi na Shule ya sekondari Makamba iliyopo Mabibo.

Kando ya uboreshwaji wa miundombinu ya Barabara kata hiyo pia kupitia fedha za ndani imeimarisha miundombinu ya masoko ambapo masoko mawili katika kata hiyo yanajengwa ambapo soko la kwanza lipo mtaa wa Kimanga lililokamilika kwa asilimia tisini na soko lingine lipo mawenzi Darajani lipo katika hatua za awali za ujenzi.

Kwa upande wa shule kata hiyo imeboreshewa shule yake ya sekondari imejengwa kwa ghorofa zipatazo nne na inatarajiwa kuwa na kidato cha tano itakapokamilika ambapo kwa sasa ujenzi huo pia umefikia 90%.

Aidha Kiwombya amesema kutokana na kata hiyo kutokuwa na Zahanati yake tayari hatua zimekwishachukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa zahanati yake itakayojengwa hivi karibuni katika eneo la Mawenzi ambapo kwa sasa kinachosubiriwa ni fidia kwa ambaye alikuwa anamiliki eneo hilo.

Katika uimarishaji wa chama cha mapinduzi hivi karibuni mwanzoni mwa mwezi Novemba 2023 Diwani huyo alifanya tukio kubwa la kuwapatia wajumbe wa mashina vitabu vya rejea 81, bendera za kati 81 na Bendera kubwa za mitaa sita.

Akihitimisha mahojiano yake amesema anamshukuru sana Rais Dk, Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi ya kimakakati na isiyo ya kimkakati.

No comments