Ads

WATENDAJI TARURA WATAKIWA KUFANYA MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA BARABARA KIPINDI HIKI CHA MVUA

Na Francisco Peter

Wakati Mvua kubwa zikindelea kunyesha kila mahali nchi nzima athari za mvua zimekuwa zikitokea baadhi ya maeneo ikiwemo Daraja la Jangwani kujaa tope zito na takataka na kusababisha maji kupita juu ya daraja kusababisha magari kukosa sehemu ya kupita pamoja na watembea kwa miguu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila akiambatana na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Inocent Bashungwa walitembelea eneo hilo na kujionea hali halisi barabara ikiwa imejaa matope baada ya maji kupungua huku chini ya daraja takataka zikiwa zimejaa  magari yakipita kwa shida  hivyo.

Waziri  Tawala za Mikoa na  Serikali   za  mitaa  Mohamed Mchengerwa amemuagiza Mtendaji wa Tarura na Mameneja wake kuanzia ngazi za Mikoa kutoka ofisini na kutembelea barabara zote kipindi hiki cha mvua kuangalia matatizo na kuyapatia suluhisho hata mvua zikinyesha tena kusitokee madhara.

Serikali inaendelea na jitihada za muda mfupi na mrefu kutoa suluhisho la changamoto ya sehemu hiyo amayo imekuwa kero.kila Mvua kubwa zinaponyesha ambapo hivi karibuni Benki ya Dunia World benki bao wametoa edha za mkopo kwa ajili ya ujenzi wa daraja kubwa hivyo wataalamu watakaa nao kuonesha namna desine ya daraja hilo litakavyojengwa ambapo litaangalia kipidi cha miaka 100.

"Serikali imejidhatiti kufikiria miaka 100 kwani miaka ya nyuma Mzabuni na Wataalamu waliopewa kujenga mradi huu walituangusha na ingetakiwa wapelekwe hata mahakamani kwani wamelisababishia taifa hasara kubwa na hivyo hili hatutaruhusu lijirudie tena" amesema Mchengerwa.

Sambamba na haya ametoa pole kwa wananchi waliokumbwa na Mafuriko nchi nzima na kuwaagiza Wakuu wa Mikoa yote pamoja na Wakuu wa wilaya watoke ofisi watembelee wakakague athari  za mafuriko kusaidia shughuli za wananchi waliokumbwa na adha ya mvua kwa kuwapa pole.

Kwa Upande wake Waziri wa Ujenzi Inocenti Bashungwa amesema Wananchi wanatakiwa wafahamu mabadiliko tabia nchi  mvua zinanyesha kubwa na kusababisha mafuriko na miundombinu iliyojengwa kutokana kutojua hali halisi ya hali ya hewa ijayo hivyo athari kutokea kutokana na hilo Serikali itahakikisha sasa inaangalia suala hili kwa jicho la tatu.



Katika hatua nyingine Waziri Inocenti Bashungwa na Mkuu wa Mkoa RC Albert Chalamila walitembelea Shule ya Msingi Kimbamba katika Halmashauri ya Ubungo na Kimara Bonyokwa  kukutana na kero ikiwemo ya  Maji yaliyosabishwa na mafuriko kuvuka na kuingia kafika ujenzi mradi mpya wa madarasa pia barabara ya kibamba shule kukosa alama za barabarani na kusababisha wanafunzi kugongwa na magari na pikipiki.

Waziri Mwenye dhamana Inocenti Bashungwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Tanroad kuhakikisha kero zote hiyo ya barabara kutatuliwa mara moja kwa kuweka miundombonu  wezeshi ambayo wananchi wataendelea na majukumu yao ya kukuza uchumi na kuondokana na adha ya vifo vya mama wajawazito pindi waendapo kujifungua

No comments