Ads

SHEIKH DKT. SALUM ASISITIZA UMUHIMU WA MAADILI KWA WANANDOA.

Na  Francisco Peter.

MWENYEKITI Taifa wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum amesema ili kuepuka dhambi utokanao na zinaa, wanandoa wote wawili wa kiume na kike hawanabudi kuachana na tabia mbaya ya kutoka nje ya ndoa, kwani dhambi hiyo ni kubwa kuliko wananndoa wanavyodhani ni dogo lakini wanayemkosea halioni dogo na adhabu yake siku ya kiama ni kubwa.Amesema ilikuondoa suala la kutoaminiana kwa wanandoa,  hawanabudi kuachana na taarifa za kinafiki baina yao kutoka kwa wafitini.

Hayo yalisemwa jana na Sheikh, Alhad Musa alipozungumza na mtandao huu Ofisini kwakwe mkoani Dar es Salaam kufuatia kwa wimbi kubwa la wanandoa kwenda katika vituo vya afya na hospitali kubwa kupima DNA kwakile kinachoitwa kukosekana kwa uaminifu baina ya wanandoa.

“Kwanza watanzania hawanabudi kutambua kwamba ninayoyasema ni kwa niaba ya JMAT na si vinginevyo wakati uliopita nilikuwa nina kofia mbili hii ya JMAT na ya Sheikh Mkoa wa Dar es Salaam lakini sasa nazungumza kwa niaba ya Taasisi kubwa tatizo lipo, kikubwa nikuwa na hofu ya Mungu hilo tu, tukiwa na hofu ya Mwenyezi Mungu tutakuwa salama pasipo hivyo kuiona pepo itakuwa aghalabu” alisema Sheikh Mussa.

Sheikh Mussa amesema dhambi ifanywayo na binadamu wa karne hii ni kufulu  dhiadi ya ile ya Sodoma na gomora, kwakuwa imefikia mahala sasa wanaume kwa wanaume wanahitaji kufunga ndoa kwa kile wanachokiita haki za binadamu ni upuuzi na ujinga kwa binadamu waliostaarabika ,sodoma walifanya kwa siri sasa ni bayana jambo ambalo halikubaliki mbele za Mungu.

Aidha Sheikh amesema ili kuepuka ushenzi utokanao na zinaa,wanandoa wote wawili wa kiume na kike hawanabudi kuachana na tabia mbaya ya kutoka nje ya ndoa,kwani dhambi hiyo ni kubwa kuliko wananndoa wanavyodhani, kwao ni dogo lakini wanayemkosea halioni dogo na adhabu yake siku ya kiama ni kubwa.

Pia Sheikh amesema  yapo makosa yanayofanywa na wanaume kwa hoja ambazo hazina mashiko hata kidogo mtahalani, kumbagugua au kumkataa mtoto kwa kigezo cha rangi na maumbile hivyo tu, hadi kufikia kupima DNA bahati nzuri awe wake asipo kuwa wake atakuwa ameaathirika kisaikolijia kwa kiasi kubwa.

“Siyo sahaihi kuwakataa watoto kwa kigezo cha rangi, maumbile ,kwakuwa nyakati za zamani Mtume S.A.W alijiwa na mwanamume mmoja akiomba ushari kwake kuhusu mke wake kuzaa mtoto mwenye haiba ya kifrika ilkhali wao ni waarabu, mke na mme, Mtume alimjibu Mwanaume yule yakuwa je

 “Wewe ni mfugaji ulianza na ngamia wangapi? Na je walikuwa na rangi gani? Alimjibu kwa rangi za wakati huo akajibu hubadirika badirika ,kwahiyo mtume alimjibu ndivyo Maisha yalivyo endelea kumcha Mungu” amesema.

Sheikh amesema kwamba kadhia kubwa katika wimbi hili kubwa la watu kupima DNA ni kutoaminiana baina ya wanadamu. 

No comments