Ads

TCAA KUWAKUTANISHA WADAU SEKTA YA ANGA KUADHIMISHA MIAKA 20

Na Mwandishi wetu .

KATIKA kuadhimiasha miaka 20 ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TCAA) imeandaa mjadala wa wadau wa usafiri wa Anga kwa lengo la kuwakutanisha pamoja kujadili mafanikio na chagamoto mbalimbali zilizopo katika sekta hiyo.

Mbali na mjadala huo pia kutakuwa na mbio za hisani zitakazofanyika Octoba 29 zitakazoanzia katika Viwanja vya mlimani city Jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema leo Octoba 26 kuhusiana na Maadhimisho ya miaka 20 ya TCCA, Mwenyekiti wa maandalizi ya Maadhimisho hayo Mellania Kasese amesema kabla ya mjadala huo kutakuwa na mbio hisani Kwa lengo la kutunisha mfuko wa upandaji miti katika maeneo kame.

Amesema mjadala wa wadau unatarajia kufanyika Octoba 30 katika ukumbi wa Mwalimu Julias Nyerere ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Amesema mjadala huo utatoa nafasi kwa wadau wa sekta ya usafiri wa Anga kutoa chagamoto mbalimbali wanazokubana nazo.

"Octoba 5 mwaka huu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hii aliweza kuzindua Maadhimisho haya na kuweka bayana mafanikio na chagamoto katika miaka 20 ya Maadhimisho hayo hivyo hii ni Moja ya njia ya kukutana na wadau wa sekta hii kujadiliana mambo mbalimbali "alisema Kasese.

Kasese amesema mpaka Sasa. maandalizi ya mbio hizo tayari yamekamilika tayari ambapo mbio hizo zitaanzia katika Viwanja vya mlimani city Jijini Dar es Salaam.

Aidha amesema mbio hizo zitakuwa ma urefu wa umbali wa kilometa tano mpaka kumi hivyo aliwaomba watanzania kujitokeza kwa wingi siku hiyo.

"Shamra shamra za Maadhimisho haya zimekuwa zikiendelea Kwa lengo la kuzungumzia mafanikio yaliopatikana katika miaka 20 TCCA mpaka sasa maandalizi yamekamilika vifaa vyote vimeishawasili na Octoba 30 kutakuwa na mjadala wa wasafiri wa Anga "Kasese

Naye katibu wa Chama Cha Riadhaa Mkoa wa Dar es salaam , Samweli Mwela amesema tangu awali wamekuwa walishirikiana na TCAA katika maandalizi y mbio hizo wamekuwa walishirikiana vyema katika maandalizi kutokana na Chama hicho ndio limekuwa kikiusika katika mbio zote.

"Tumejiridhisha na kupima njia zote zitakazotumika katika mbio hizo Ili kuhakikisha zinakuwa katika Hali ya usalama"alisema alisema Mwela 

Aidha alitoa wito kwa wadau wengine wanaofanya mbio za hisani kushirikiana na Chama hicho Ili kuweza kuepukana na chagamoto mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza.






No comments