Ads

MVUA KUBWA KUNYESHA GEITA, KAGERA, KIGOMA.

Mmlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa inayoweza kutokea katika baadhi ya maeneo Mikoa ya Kagera, Geita pamoja na Kigoma kwa muda wa siku tano kuanzia leo Oktoba 19 - 23, 2023.

TMA imeeleza kuwa uwezekano wa kutokea mvua hizo pamoja na athari zinazoweza kujitokeza ni wastani.

Athari zinazoweza kutokea ni baadhi ya makazi kujaa maji pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za uchumi.


No comments