Ads

MWENYEKITI wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga Tanzania

MWENYEKITI wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga Tanzania (SIUMA), Mkoa wa Dar es Salaam Yusuph Namoto amesema wameanza opereshesheni ya safisha Dar es Salaam kwakuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya bishara ya kutumia majiko na mitungi ya gesi sehemu ambazo siyo rasmi katika masoko mbalimbali mkoani humo.

Namoto aliyasema hayo alipofanya mahojiano na HabariLEO katika ofisi za Shiuma zilizopo Kariakoo nakueleza nia na dhamira ya kufanya hivyo kwamba sababu kubwa nikuepuka athari zinazoweza kusababishwa na mlipuko utokanao na moto.


“Operesheni hii ni endelevu na inafanyika Dar es Salaam nzima ambapo kama ulivyoshuhudia kuanzia Novemba 8, 2023 operesheni hiyo imeanza kwakukamata wafanyabiashara wenzetu ambao wanafanya biashara zinzaotumia mioto kwenye maeneo ambayo siyo rasmi katika maeneo mbalimbali ya masoko ya Dar es Salaam” alisema Namoto.

Akizungumzia maeneo hayo Namoto aliisema siyo tengefu kwa ajili ya biashara zinazohusisha mapishi kwa mfano kandokando mwa meza au vizimba vya wafanyabishara watu wanakaanga mihogo, chipsi na mapishi ya vyakula mbalimbali jambo ambalo halikubaliki.


“Masoko yetu yote yana vitengo mbalimbali matharani matunda, mamalishe na babalishe, matunda na mbogamboga na wanapangwa kwa mujibu wa taratibu za masoko husika lakini kwa bahati mbaya sana kumeibuka utaratibu usiofaa ambao wakati mwingine husababisha mlipuko wa moto na kuleta athari ya kuungua kwa masoko nchini hivyo tumeona tulekezane na tumelekezana lakini bado baadhi wamekuwa wa babaifu na hivyo kuamua kufanya operesheni hii ambapo majiko yao ya kiwemo ya gesi na ya mkaa kuchukuliwa na kupelekwa mahakama ya jiji ambako watayakomboa kwa faini” alisema Namoto

Sanjari na Operesheni hiyo Namoto aliwataka wafanyabiashara kufuata sheria za masoko wanayofanyia biashara bila shuruti ikiwemo kutokupanga bidhaa chini na badala yake wapange bidhaa zao kwenye meza kama sehemu ya vizimba vyao.

“Kwakufanya hivyo watakuwa wamethaminisha na kubidhaisha biashara zao na zitakuwa na thamani na kuuzika kwa walaji, si utaratibu unaofaa kwa masoko ya kisasa na ya kimataifa kupanga bidhaa chini kama kuna changamoto za kiutendaji ofisi zetu zipo wazi wakati wowote watuone” alisema Namoto

Miongoni mwa wafanyabiashara waliohojiwa na HabariLEO katika masoko ya Kariakoo na Mchikichini walisema operesheni hiyo inapaswa kuwa endelevu na siyo Dar es Salaam tu bali nchi nzima.

“Naitwa Najima Said nafanya biashara ya nguo za Watoto na soksi napongeza Operesheni hii na iwe endelevu masoko yetu ni ya kimataifa kuweka bidhaa chini na kupikapika hovyo ni mambo yaliyopitwa na wakati kwa nchi yetu tupo ngazi au kiwango cha Kimataifa tunapokea mataifa yote ya Afrika Mashariki bado tunapanga chini utadhani tupo gulioni? “ alisema Najima

No comments