Ads

WACHUNGAJI WATAKIWA KUISHI MAISHA YA KUMPENDEZA MUNGU

Assemblies of God Tanzania (EAGT) Jimbo la Temeke, Aidan Mabuga amewataka watumishi wa Mungu hususani wahubiri waishi yale wanayoyafundisha.

Ushauri huo umetolewa jana Novemba 11, 2023 na askofu huyo alipokuwa akizungumza na HabariLEO katika Kanisa la EAGT Mlima wa Faraja mtaa wa Sandali wilayani Temeke Dar es Salaam.

“Akinukuu kitabu cha 1 Wakorintho 11:1 ambapo Mtume Paulo aliwaandikia Wakorintho akisema nifuateni mimi,kama mimi ninavyomfuata Kristo, kwa maana hiyo yatupasa kuwa kielelezo kwa waumini kwakutenda yaliyo mema na ya kumpendeza Mungu kwakufanya hivyo tutakuwa tumeungana na Kristo Yesu Masia” alisema Askofu Mabuga.


Askofu huyo aliyasema hayo katika mahojiano na HabariLEO ambapo kunafanyika mkutano wa kiinjili katika kanisa la EAGT Mlima wa Faraja kuanzia Novemba 7, 2023 na mkutano huo utatamatika leo Novemba 12 katika viunga vya viwanja vya Binti Musa.

Kwa mujibu wa Askofu Mabuga ni kwamba agenda kubwa ya Mkutano huo ilikuwa ni, wa mambo makubwa mawili, la kwanza ni watu kutubu dhambi zao na kumgeukia Mungu na la pili ni maombi ya kifamilia yenye lengo la kurejesha amani ndani ya familia.

“Dhumuni na malengo makubwa kama nilivyosema jamii imrudie Mungu kwa kufanya hivyo Taifa na ulimwengu utakuwa salama na jambo la msingi ni kurejesha amani ndani ya familia zetu ambapo msingi na kielelezo kikubwa kipo kwa wanandoa yaani wazazi, hawa wakipendana na kuishi kwa upendo hata Watoto watakuwa katika upande salama kwa maana Mungu anasema anachukia wanandoa kuachana” alisema Askofu Mabuga.

Askofu Mabuga alisema kwamba ili Watoto wetu waepukane na athari mbalimbali mbali jamii kwa ujumla imrudie Mungu kwakufanya ibada na kutubu kwakufanya hivyo Watoto hawatabakwa, kulawitiwa na kuingia kwenye mitego ya mmomonyoko wa Maaadili.

“Nayasema haya kwakuwa laana inayo waandama Watoto wetu kwa sasa ni zaidi ya sodoma na Gomola Watoto wetu wanawindwa na muovu shetani kama digidigi ni wakati wa Kanisa na serikali kukemea vitendo hivyo vya uzalilishaji Watoto kingono na kuweka sheria kali dhidi ya wanaojihusisha na dawa za kulevya hususani wafanyabiashara wa mtandao huo” alisema Askofu Aidan


No comments