Ads

Carbon inalenga kupunguza na kuifadhi wa hewa faida zake zatajwa kunufaisha Taifa

Francisco Peter

Imeelezwa kuwa Tanzania inanufaika na Biashara ya Carbon ambapo shughuli mbalimbali za binadamu zinaongeza viwango vya matokeo ya hewa hiyo.

Serikali imesema tayari wakaazi wa Mkoa wa Tanga wameanza kunufaika na Bishara hiyo ambapo huku ikitajwa kuwa zaidi ya Shilingi Bilion moja zimeweza kupatikana .

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo Waziri wa Mali Asili na Utalii Angela Kairuki amesema vijiji nane villkivyopo katika mkoa wa Tanga wameweza kujenga hospitali kupitia Mradi huo.

"Fedha hizo zimetokana na Miradi mbalimbali ikiwemo uhifadhi wa hewa carbon imesajaliwa ambapo zaidi ya Bilioni 20 zimepatikana kutokana na Carbon"Alisema waziri Angela Kairuki.

Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa Africa Carbon Agency Cosmas Tungaraza amesema kuwa kampuni yake imelenga kupambana na hewa ya Ukaa,Ambapo biashara ya carbon inalenga uhifadhi wa hewa hiyo.

"Biashara ya Carbon inalenga kupunguza na kuifadhi wa hewa ya ukaa,"amesema huyo wa uendeshaji Africa Carbon Agency Cosmass Tungaraza.





No comments